RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakimsikiliza mkulima wa zao la Karafuu Bw.Ali Ahmed walipofika katika kambi ya uchumaji na uchambuaji wa zao la Karafuu,katika Kijiji cha Bagamoyo Mtambwe, akiwa katika ziara yake kuangalia maendeleo ya uchumaji wa Karafuu Pemba, na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe.Salama Mbarouk Khatib na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Mkewe Mama Mariam Mwinyi,Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.Mhe.Salama Mbarouk Khatib,Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwa Rais) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban,wakimsikiliza mkulima wa zao la Karafuu Bw.Said Salim Ali, akizungumza na kutoa changamoto, wakati wa ziara ya kutembelea kambi hiyo ilioko katika Kijiji cha Bagamoyo Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika zoezi la uchambuaji wa Karafuu katika Kambi ya Bw.Said Salim Ali (kulia kwa Rais) na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe. Salama Mbarouk Khatib na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaban.(Picha na Ikulu)
WANANCHI wa Bagamoyo Mtambwe wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akizungumza na wakulima wa zao la Karafuu alipotembelea kambi ya uchumaji na uchambuaji wa karafuu ya Bw.Ali Ahmed na Bw.Said Salim Ali katika kijiji cha Bagamoyo Mtambwe Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.(Picha na Ikulu)
WANANCHI wakishiriki katika zoezi la uchabuaji wa zao la Karafuu katika Kambi ya Bw.Said Salim Ali, katika Kijiji cha Bagamoyo Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba Mkoa wa Kaskazini Pemba.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wakulima wa zao la Karafuu katika Kijiji cha Bagamoyo Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba wakati wa ziara yake kutembelea Kambi ya Bw.Said Salim Ali na Bw.Ali Ahmed.na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi.Mhandisi Zena Ahmed Said na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe. Salama Mbarouk Khatib.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Hati ya kumiliki shamba la Mikarafuu Bi.Fatma Abdulrahaman Said, wakati wa ziara yake katika kutembelea Kambi ya Uchumaji wa Karafuu Bagamoyo Mtambwe na (kkushoto kwa Rais) Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Umwagiliaji Maliasili na Mifugo.Bi.Maryam Juma Sadala.(Picha na Ikulu)
No comments :
Post a Comment