Monday, August 23, 2021

Wizara Ya Kilimo Yahimiza Wadau Kushirikiana Na Wizara Katika Upatikanaji Wa Pembejeo

 

Judica Omary kwa niaba ya waziri wa kilimo akifungua kibao kuonyesha ishara ya kufunguliwa kwa duka moja la pembejeo za kilimo katika kijiji cha Igima kwa niaba ya maduka mengine 29 yanayopatikana katika mikoa ya kusini.
Baadhi ya viongozi wakipata maelezo ya bidhaa za pembejeo zinazopatikana katika maduka ya one acre fund.
Katibu tawala wa mkoa wa Njombe Judica Omary akizungumza na wananchi wa kijiji cha Igima kwa niaba ya waziri wa kilimo katika uzinduzi wa maduka ya pembejeo.Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wizara ya Kilimo nchini inahimiza wadau mbali mbali wa kilimo kushirikiana na wiazara hiyo katika kutekeleza shughuli zinazohusiana na kilimo pamoja na upatikanaji wa pembejeo

Aidha waziri wa kilimo Prof Adolf Mkenda amesema serikali imedhamiria kuboresha sekta ya kilimo ikiwemo upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa bei nafuu na masoko ya mazao ya uhakika kwa kuendelea kuwaalika wadau mbambali wa kilimo kuja kuwekeza Tanzania.

Hayo yamebainishwa na katibu tawala wa mkoa wa Njombe Judica Omary kwa niaba ya waziri wa kilimo katika uzinduzi wa mpango wa utoaji wa pembejeo na elimu kwa duka model ulioambatana na uzinduzi wa maduka 30 ya pembejeo za kilimo kutoka kampuni ya ekari moja moja Tanzania Limited (One acre fund) uliofanyika katika kata ya Igima wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe na kuahidi kuwa serikali itaendelea kushirikiana vyema na wadau hao katika kuwasaidia wakulima kama ilivyokuwa tangu miaka 8 ya kuanzishwa kwa kampuni hiyo nchini Tanzania.

“Wizara inahimiza wadau wote wa kilimo kushirikiana na wizara yetu katika kutekeleza shughuli za kilimo na maswala mbali mbali ya upatikanaji wa pembejeo,huduma za ugani uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo na utafutaji wa masoko ya uhakika ya wakulima”alisema Judica Omary

Kuhusu bei ya mahindi amesema “Bei ya mahindi kuwa ndogo alishatoa maelezo  waziri na kwa jinsi hiyo NFRA kwa maghala yaliyopo hapa Njombe wameshaanza kununua mahindi kwa bei ya shilingi 500 kwa kilo na ni fursa ya kuanza kuchangamkiwa na kwa hapa Wanging’ombe wapo Ilembula”

Mkurugenzi wa kampuni ya ekari moja Tanzania LTD (One acre fund) Jennifer Lindgren amesema mpango huo wa kuanzisha maduka 30 ya pembejeo hapa nchini umelenga kuongeza wigo katika kilimo kwa watanzania huku wakiwa wamejikita zaidi kwa mikoa ya kusini na mkoa wa Njombe ukiwa na maduka ya pembejeo za kilimo zaidi ya 15 ikiwemo kijiji cha Igima.

“Kwa kufungua maduka tunakusudia kuwa na huduma bora na kuwafikia wakulima wengi zaidi na kampuni ya one acre fund ni muwekezaji wa uhakika nchi na tunaamini mchango wetu katika kukuza uchumi ni kielelezo tosha katika nia ya kuendeleza kilimo kwa nafasi ndogo tuliyonayo”alisema Jennifer Lindgren

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe,mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Lauteri Kanoni amesema anatarajia kuona tija katika sekta ya kilimo inaongezeka kupitia shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo.

“Niwashukuru sana kwa namna wanavyoshirikiana na wakulima wetu na kwa kadri nilivyopitia maonesho na bidhaa walizonazo ninaamini changamoto ya pembejeo itapungua kupitia kampuni hii”alisema Kanoni

Asteria Kitalula na Ibrahim Nziku  ni baadhi ya wakulima ambao wamekiri kunufaika na pembejeo hizo licha yakuwapo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa soko la uhakika la mazao yao kauli iliyoungwa mkono na diwani wa kata ya Igima paulina Samata.


No comments :

Post a Comment