Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Bi. Saada Mkuya wakiongea na waandishi wa habari hii leo Vuga – Zanzibar. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Bw. Thabit Faina na Bw. Khalid Amran Mratibu Mkuu wa Shughuli za SMZ –Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hii leo Vuga - Zanzibar kuelezea vikao vya kushughulikia masuala ya Muungano vitakavyofanyika Zanzibar tarehe 23-24 Agosti 2021. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mohammed Khamis Abdulla.
MAKAMU WA RAIS KUONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA PAMOJA YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (SMT) NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR (SMZ), ZANZIBAR
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Selemani Jafo amesema tangu kuanzishwa kwa utaratibu wa kushughulikia hoja za Muungano kupitia vikao vya Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ mwaka 2006, hoja 25 zimejadiliwa na mpaka sasa hoja saba (7) zimepatiwa ufumbuzi na hoja kumi na nane (18) zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi.
Waziri Jafo ameyasema hayo hii leo Zanzibar wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelezea kuanza kwa vikao ngazi ya Mawaziri na Kikao cha Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ kitakachofanyika kuanzia tarehe 24/08/2021 katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul – Wakil, Kikwajuni chini ya Uenyekiti wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zimeweka utaratibu wa kutatua changamoto za Muungano kupitia mfumo rasmi wa Vikao vya Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ ya kushughulikia Masuala ya Muungano” Jafo alisisitiza.
Amesema kuwa baada ya kikao cha Mawaziri wa SMT na SMZ, wajumbe watapata fursa ya kutembelea miradi ya kimkakati ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (Terminal III) na kiwanda cha Maziwa cha Bakhresa ambayo ni miongoni mwa hoja za Muungano ambazo zimekuwa zikitafutiwa ufumbuzi na
Vikao vya Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ hufanyika katika ngazi tatu ambazo ni:- Makatibu Wakuu wa SMT na SMZ, Mawaziri wa SMT na SMZ na kikao cha Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ, ambacho Mwenyekiti wake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lengo la kuweka utaratibu huu ni kuimarisha Muungano kwa kuhakikisha changamoto zote zinatafutiwa ufumbuzi wa kudumu.
No comments :
Post a Comment