Friday, August 20, 2021

WANAWAKE WAHASIBU TANESCO WASHIRIKI KONGAMANO ZANZIBAR

Wahasibu wanawake wa TANESCO  wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kongamano la kitaaluma la wahasibu wanawake TAWCA  linaloendelea katika Hotel Verde Visiwani Zanzibar.
Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar akihutubia  katika  kongamano la wahasibu wanawake wa Tanzania TAWCA  linaloendelea katika Hotel Verde  visiwani Zanzibar.


WANAWAKE Wahasibu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wameshiriki kongamano la kitaaluma la wanawake wahasibu linalofanyika katika hotel ya Verde Zanzibar. 

Kongamano hilo la nne limefunguliwa  Agosti 19, 2021 na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali  ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdallah akimwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ally Hassan Mwinyi.

TANESCO imefadhili kongamano hilo lengo likiwa ni kuwakutanisha wahasabu wanawake wa TANESCO na wataalamu wengine wa kada hiyo kutokana na makongamano kuwa sehemu mahususi ya kuzungumzia masuala ya kada ya husika.

No comments :

Post a Comment