Wednesday, July 7, 2021

TUTAENDELEA KUONGEZA UZALISHAJI WA BIDHAA YETU 'SARUJI' KUENDANA NA MAHITAJI YANAYOKUA KWA KASI KATIKA SOKO-DANGOTE


Afisa mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Dangote Abdullahi Baba akizungumza na Waandishi wa Habari katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 45 yanayaoendelea jijini Dar es Salaam,akieleza namna bidhaa yao 'saruji' inayotengenezwa na kampuni hiyo ilivyopokelewa vyema na Watanzania na kwamba mahitaji yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku .
Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Dangote,Davis Kambi (wa pili kulia) akifafanu jambo kwa mmoja wa wateja waliofika kwenye banda la kampuni hiyo katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 45 yanayaoendelea jijini Dar es Salaam,ambapo amesema kuwa Kiwanda hicho kipo kwa ajili ya kujenga Tanzania na kutokana na ushirikiano wanaoupata wana mkakati mkubwa wa kusambaza saruji nchi nzima
Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Dangote,Davis Kambi akizungumza na Waandishi wa Habari katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 45 yanayaoendelea jijini Dar es Salaam,ambapo amesema kuwa Kiwanda hicho kipo kwa ajili ya kujenga Tanzania na kutokana na ushirikiano wanaoupata wana mkakati mkubwa wa kusambaza saruji nchi nzima.

  Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Dangote kimesema kitaendelea kuongeza

uzalishai wa bidhaa hiyo muhimu kwa ajili ya ujenzi ili kuendana na mahitaji yanayokua kwa kasi katika soko la Tanzania


Akizungumza na Waandishi wa habari katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 45 yanayaoendelea jijini Dar es Salaam, Afisa mtendaji Mkuu Abdullahi Baba alisema saruji inayotengenezwa na kampuni hiyo imepokelewa vyema na Watanzania na kuongeza kuwa mahitaji yamekuwa yakiongezeka kwa kasi.

Alisema tangu kiwanda hicho kianze kufanya kazi mwaka 2015 kimekuwa kikijikita katika kutengeneza bidhaa bora lakini zenye gharama nafuu lengo likiwa pia ni kuwawezesha Watanzania kumiliki nyumba

‘Kumekuwepo na uwekezaji mwingi na mikubwa ya miundo mbinu hapa Tanzania na Dangote tumekuwa ni moja kati ya wazalishaji wakubwa kuliko wengine wote wa saruji kwa ajili ya miradi hii. Tunayo furaha kutoa mchango wetu katika maendeleo ya miundo mbinu kwa hapa Tanzania, ‘

Alisema Dangote inaona Tanzania kama sehemu muhimu ya biashara yake kutokana na hatua mbali mbali zinazochukuliwa na Serikali katika kuweka mazingira bora ya uwekezaji ambayo yanaipa nguvu kampuni hiyo kuendelea kuwekeza,

‘Tumeshaanza kuongeza uzalishaji wetu na tutaendelea kuongeza zaidi na zaidi kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na saruji ya kutosha. Mazingira ni rafiki na tunapenda kuuhakikishia umma kuwa Dongote ipo na itaendelea kuwepo,’

Afisa Mtendaji Mkuu huyo aliongeza kuwa Dangote Cement pia ina mipango ya kuzalisha saruji na kuiuza katika siku za usoni na kuongeza kuwa kiwanda hicho kina uwezo mkubwa wa kuzalisha saruji kwa ajili ya matumizi ya ndani na nje.

KIWANDA cha saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara kimeishukuru Serikali kwa kutoa ushirikiano wa hali ya juu katika kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora zinazotolewa na kampuni hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Dangote,Davis Kambi alisema kuwa Kiwanda hicho kipo kwa ajili ya kujenga Tanzania na kutokana na ushirikiano wanaoupata wana mkakati mkubwa wa kusambaza saruji nchi nzima na wamejikita katika kuelimisha na kuwaaminisha Watanzania kuhusu ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho kikubwa nchini.

"Katika maonesho haya kiwanda chetu kimejikita katika kuelimisha Watanzania kuhusu bidhaa ya saruji 'Dangote Cement' inayozalishwa na kiwanda chetu,kwa hiyo kupitia maonesho hayo tutaendelea kuelimisha Umma kuhusiana na bidhaa zetu zinazopatikana nchi nzima" alisema Davis.

Vilevile aamesema kuwa kwa sasa wanasambaza saruji nje ya mipaka ya Tanzania ikimemo katika nchi za Rwanda Burundi na wamejipanga kusambaza bidhaa hizo katika nchi za Comoro na Madagascar na hiyo ni kutokana na kuongezeka kwa kasi ya uzalishaji.

No comments :

Post a Comment