Mkurugenzi
Mtendani wa Taasisi ya Peace Life for Person with Disability Foundation
(PLPDF), Sophia Mbeyela, Lita Paulsen wakiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi pamoja na wadau wa maendeleo ya wanafunzi wenye ulemavu mara
baada ya kuzindua kampeni ya ujenzi wa Vyoo rafiki kwa wanafunzi wenye
ulemavu mashuleni. Kampeni hiyo imeziduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendani wa Taasisi ya Peace Life for Person with Disability Foundation
(PLPDF), Sophia Mbeyela akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa
vyoo rafiki kwa wanafunzi wenye Ulemavu mashuleni leo Julai 14,2021.
Kulia ni balozi wa kampeni ya Vyoo rafiki Mlinzi wa Afya yangu, Lita
Paulsen.
Balozi
wa kampeni ya Vyoo rafiki Mlinzi wa Afya yangu, Lita Paulsen
akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa vyoo rafiki kwa wanafunzi
wenye Ulemavu mashuleni leo Julai 14,2021 jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
TAASISI
ya Peace Life for Person with Disability Foundation (PLPDF) yazindua
kampeni ya ujenzi wa vyoo rafiki kwa wanafunzi wenye Ulemavu mashuleni
leo Julai 14, 2021 katika mgahawa wa Lavent Masaki jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi Mtendani wa Taasisi ya
Peace Life for Person with Disability Foundation (PLPDF), Sophia Mbeyela
Maarufu kama Madam Sophy amesema kuwa vyoo rafiki ni Mlinzi wa Afya
hivyo ameiomba serikali na jamii kwa ujumla kuunga mkono kampeni hiyo
kwa kuchangia katika Ujenzi wa vyoo mashuleni kwaajili ya matumizi ya
wanafunzi wenye ulemavu.
Amesema
kuwa Unaweza kuchangia kupitia namba ya M-Pesa 55557777 huku namba ya
Akaunti ya Benki ya NMB 22510027964 kwa jina la PLPDF.
"Lengo
la kuzindua kampeni hii ni kutaka kujenga vyoo rafiki kwa wanafunzi
wenye ulemavu, kampeni hii itakuwa endelevu kwani tumeona changamoto ya
vyoo rafiki mashuleni, tunataka wanafunzi walemavu walio mashuleni
wasome bila kuwa na changamoto.
Changamoto
hii nimeona katika shule ya Sekondari Jangwani nilitembelea nakuona
vyoo vichache na wanafunzi ni wengi, Kama Jangwani ambayo ipo Mjini
inachangamoto ya vyoo rafiki kwa wanafunzi, je huko vijijini itakuwaje?"
Amehoji Sophia.
"Ukubwa
wa Changamoto hii tumeanza kuona katika shule ya sekondari ya Jangwani
ambapo kunawanafunzi 84 lakini kunamatundu ya choo ambayo ni rafiki ni
manne (4) tuu. Lakini katika manispaa ya Ilala ina shule 17 zenye
wanafunzi mchanganyiko na wanafunzi wenye ulemava lakini hazina vyoo
rafiki kwa wanafunzi hao." Amesema Sophia
Hata
hivyo Sophia amesema kuwa anaungana na wadau wengine wa afya na
maendeleo kwaajili kuchangia ujenzi wa vyoo katika manispaa ya Ilala
katika shule ya Sekondari ya Jangwani jiji la Dar es Salaam pia ujenzi
wa vyoo rafiki kwa walemavu utaendelea katika mikoa mingine.
Licha
ya hayo amesema kuwa kama kampeni hiyo itafanikia zaidi katika mkoa wa
Dar es Salaam kampeni hiyo itaendelea katika shule nyingine katika
wilaya nyingine hapa nchini na baadae tutendelea kutoa elimu jumuishi
kwa wanafunzi walemavu juu ya suala la kuwa na vyoo rafiki kwa mahitaji
ya wanfunzi wenye ulemavu.
Amesema
kuwa watahakikisha wanafunzi wenye ulemavu wanasoma katika mazingira
mazuri, hiyo wanaomba wadau, serikali pamoja na jamii kwa ujumla kuweza
kuungana na Taasisi ya Peace Life for Person with Disability Foundation
(PLPDF) katika kufanikisha lengo la kuwasaidi wanafunzi wenye ulemavu
walioko mashuleni ili wapate elimu bora katika mazingira mazuri zaidi.
Kwa
Upande wa mgeni Rasmi ambaye ni balozi wa vyoo rafiki mlinzi wa afya
yangu, Lita Paulsen amesema ameisa jamii kuunga mkono kampeni ya Sophia
kwaajili ya kusaidia wanafunzi wenye ulemevu mashuleni.
Amesema
kuwa sio lazima mtu achangie pesa bali anaweza kuchangia mawazo au vitu
vitakavyowezesha kujenga vyoo rafiki kwa watu wenye ulemavu. Madam Lita
amesema kuwa choo kimoja kinagharimu shilingi milioni sita hadi saba
tuu hivyo amewaomba wadau kujitoa kwaajili ya hilo ili kuwezesha
wanafunzi wenye ulemavu waweze kufikia malengo yao.
Kwa
upande wake Afisa Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam, Kagemulo
Runyoro amesema kuwa serikali imetoa ushirikiano wa hali ya juu kwa
kutoa eneo ambalo litakwenda kujengwa vyoo rafiki kwa waafunzi wenye
ulemavu pia na vibali vingine vyote ambavyo vitatakiwa.
Amesema
kuwa pia watajitahidi kutafuta wadau katika kuchangia kampeni ya
kujenga vyoo rafiki kwa wanafunzi wenye ulemavu mashuleni.
"Nikweli
kumekuwa na hali ambayo sio rafiki kwa wanafunzi walemavu hususani
majengo, madarasa, ofisi na vyoo zimekuwa sio rafiki kwa watu wenye
ulemavu, tutajitahidi kuweka hali nzuri kwa watu wote." Amesema Kagemulo
Nae
Mwali Chavala Mariam amesema kuwa Miundombinu katika shule ya Sekondari
Jangwani kwa wanafunzi wenye ulemavu sio rafiki pamoja na mahitaji
mengi waliyonayo na changamoto walizonao, choo ni kitu mhimu zaidi ili
mtu aishi salama na kwa afya yake.
"Sisi
tunatoa wito kwa taasisi mbalimbali mashirika mabalimbali, makampuni na
serikali kila mtu aguswe aone kwamba leo ama kesho anamtoto mlemavu
tuchangie ili watoto hawa wajengewe vyoo ambavyo ni rafiki kwao."
Amesema Mwalimu Chavala.
Hata
hivyo Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Jangwani, Aisha Ahmed amesema
kuwa kampeni hii itakavyofanikiwa itasaidi wanafunzi wengi zaidi wenye
ulemavu. "Itatatua changamoto zilizopo za vyoo rafiki katika shule na
sisi tutazidi kupata maarifa ya elimu bila kikwazo na kuweza kuwa na
usiri pale tutakapokuwa na shida ya kwenda chooni."
Pia
ameiomba Serikali na mashirika yasiyoyakiserikali na yakiserikali
kuchangia kampeni iliyoanzishwa na Sophia kwaajili ya kusaidi watu wenye
ulemavu hapa nchini ili wanafunzi wenye ulemavu kupata elimu bila
vikwazo.
No comments :
Post a Comment