Wednesday, July 14, 2021

MAKAMU WA RAIS KUANZA ZIARA KIGOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hapo kesho Julai 15, 2021 anatarajiwa  kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Kigoma.

 Katika ziara hiyo, Makamu wa Rais anatarajia kuweka mawe ya msingi katika ujenzi

wa miradi mbalimbali ikiwemo kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme eneo la Nguruka,  jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Ualimu Kabanga, jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Mji wa Kasulu, jiwe la msingi  ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Uvinza pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Kakonko.

 Aidha Makamu wa Rais atazindua  Miradi mbalimbali ikiwemo ya Afya , Kufungua jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Mkoa wa Kigoma, kukagua maendeleo ya baadhi ya miradi katika mkoa huo pamoja na kuwasalimu wananchi katika maeneo mbalimbali atakayotembelea.

No comments :

Post a Comment