Mtaalam wa maabara wa MSD Joseph
Kitukulu, akiwaonesha moja ya mashine zinazonunuliwa na MSD baadhi ya
madaktari na Wataalam wa Maabara wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili,Mloganzila wakati akiwatambulishwa mashine na vitendanishi vya
maabara vipya vinavyonunuliwa na Bohari ya Dawa (MSD) kwa matumizi ya
vituo vya kutolea huduma za afya vya serikali nchini.
Utambulisho wa vifaa hivyo ukiendelea. Vifaa hivyo vinapima
hematolojia(full blood picture), kemia ya mwili(body chemistry), wingi
wa damu(hemoglobin), sukari(glucose), mkojo(urinalysis) na vichocheo vya
mwili(hormones)
Msimamizi wa Utekeleza Mpango Mkakati wa MSD, Bi. Neema Mwale,
akizungumza na wataalamu hao kuhusu hatua ya MSD kununua vifaa hivyo
kutoka kwa wazalishaji na jinsi inavyochangia juhudi za serikali
kuboresha huduma za afya za wananchi, na kuipunguzia serikali gharama
kwa asilimia 40 hadi 50
Na Mwandishi Wetu.
BAADHI ya madaktari na Wataalam wa Maabara wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili,Mloganzila wametambulishwa mashine na vitendanishi vya maabara
vipya vinavyonunuliwa na Bohari ya
Mtaalam wa maabara wa MSD Joseph Kitukulu amewaeleza kuwa, mbali na vifaa hivyo kutumia teknolojia ya kisasa,kupunguza muda na kuwa na gharama nafuu vinauwezo wa kuchukua sampuli nyingi zaidi.
Kwa upande wake,Msimamizi wa Utekeleza Mpango Mkakati wa MSD, Bi. Neema Mwale amesema kuwa hatua ya MSD kununua vifaa hivyo kutoka kwa wazalishaji itachangia juhudi za serikali kuboresha huduma za afya za wananchi, na kuipunguzia serikali gharama kwa takribani asilimia 40 hadi 50
No comments :
Post a Comment