Mhandisi
Mkazi wa Mradi wa Uzalishaji Umeme wa Maji wa Julius Nyerere, Eng. John
Mageni (kushoto) akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi kwa Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (wapili kulia) na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (watatu kulia)
wakati ujumbe wa benki hiyo ulipotembelea mradi huo unaofanyika katika
bonde la mto Rufiji. Wa mwisho pichani ni Naibu Mkurugenzi wa Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO), Eng. Pakaya Daniel.
Mhandisi
Mkazi wa Mradi wa Uzalishaji Umeme wa Maji wa Julius Nyerere, Eng. John
Mageni akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati ujumbe wa benki hiyo
ulipotembelea mradi huo unaofanyika katika bonde la mto Rufiji. Kushoto
ni Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme, Eng. Pakaya Daniel na Wajumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati) akiteta jambo na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme, Eng. Pakaya Daniel wakati
ujumbe wa benki hiyo ulipotembelea mradi huo unaofanyika katika bonde
la mto Rufiji. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya
CRDB, Dkt. Ally Laay.
Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme, Eng. Pakaya Daniel akizungumza na ujumbe wa benki ya CRDB uliotembelea Mradi wa Uzalishaji Umeme wa Maji wa Julius Nyerere wa unaofanyika katika bonde la mto Rufiji.
No comments :
Post a Comment