Kampuni ya madini ya Barrick
inashiriki katika maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 45
yanayaoendelea jijini Dar es Salaam ambapo banda lake la maonyesho na
wajasiriamali inaowawezesha kutoka vijiji jirani na mgodi wa Bulyanhulu
mkoani Shinyanga linaendelea kuwavutia wananchi na viongozi mbalimbali
na wadau wa sekta ya madini.
Mmiliki wa mgodi wa madini ya
Tanzanite,bilionea Laizer Saniniu,(wa tatu kutoka kulia) akiwa na
wafanyakazi wa Barrick na wajasiriamali wanaowezeshwa na kampuni hiyo
baada ya kuwatembelea katika maonesho ya Sabasaba jijini Dar es salaam.
Mfanyabiashara wa madini,Laizer Saniniu (Kulia) akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea banda la maonesho la Barrick.
Waziri wa Ardhi,Mh.William
Lukuvi,(kulia) akiongea na Wafanyakazi wa Barrick alipotembelea banda la
kampuni hiyo kwenye maonesho ya Sabasaba.
Naibu Waziri wa Biashara na
Viwanda,Dk.Exaud Kigahe(Kulia)akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na
wajasiriamali wanaowezeshwa na kampuni ya Barrick.
No comments :
Post a Comment