Saturday, June 19, 2021

WAZIRI WA AFYA AFANYA KIKAO NA WATUMISHI WAKE KUTEKELEZA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Waziri wa Afya Dkt.Dorothy Gwajima akiongea na watumishi wa Wizara ya Afya Kwenye viwanja vya wizara Kwenye mji wa Serikali Mtumba Kwenye Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Leonard Mchau akiongea wakati wa kikao hicho ambacho kilikuwa na lengo la kusikiliza changamoto za watumishi
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Idara Kuu Afya Bi.Deodatha Makani  akiwa Kwenye kikao hicho
Mmoja wa watumishi wa Wizara hiyo akichangia wakati wa kikao Cha Waziri wa Afya na watumishi wa Wizara hiyo ikiwa ni kutekeleza Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma

Baadhi ya watumishi waliojitokeza Kwenye kikao Cha Waziri Dkt.Gwajima wakifuatilia   wakati Waziri akiongea
Watumishi wa Idara Kuu Afya na Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Waziri wao wakati wa kikao Cha pamoja kilichofanyika Leo jijini Dodoma

 Picha ya pamoja ya Waziri Dkt.Gwajima akiwa na watumishi wa Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Mara baada ya kumalizia kikao hicho

Picha ya pamoja ya Waziri wa Afya,viongozi na baadhi ya watumishi wa Idara Kuu Afya

Na.Catherine Sungura,Dodoma

Viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wametakiwa kuwa na utaratibu wa vikao kila baada ya miezi mitatu pamoja na mawaziri wao kwa lengo la kujadili mafanikio na changamoto na kuziwekea mpango wa pamoja wa kuzipatia majibu.

Rai hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima  wakati wa kikao chake na watumishi wa Idara mbili zilizopo Kwenye wizara yake(Afya na Maendeleo ya Jamii) Cha kusikiliza na kutatua changamoto zinazoikabili wizara hiyo zikiwemo za watumishi hao.

Mkutano huo ambao umefanyika Kwenye viwanja vya wizara hiyo zilizopo Kwenye mji wa Serikali Mtumba ikiwa ni Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza tarehe 18-23 Juni, 2021.

Dkt.Gwajima amesema anatamani kuona wizara hiyo inakuwa ya mfano wa katika kutambua na kuzipatia majibu changamoto zinazowakabili watumishi wake na wateja wake hivyo, amewataka wakurugenzi kuweka utaratibu wa kukutana kila baada ya miezi mitatu.

"Changamoto nyingi zinaweza kutatuliwa ndani na viongozi  yaani zipo ndani ya uwezo wetu kinachohitajika ni uratibu baina yetu, hivyo upo umuhimu wa kukaa pamoja kila baada ya miezi mitatu na kuongea na watumishi wetu kwa ajili ya kuchota mawazo na uzoefu".Alisisitiza

Hata hivyo  Dkt. Gwajima aliwataka watumishi hao kuwajibika na kuwa waadilifu wanapotekeleza majukumu yao na pia kutengeneza mfumo ambao utawajenga watumishi hao katika utumishi wenye viwango stahiki vya kitaifa na kimataifa.

Akielezea kaulimbiu ya mwaka huu inayosema "Kujenga Afrika tunayoitaka, kupitia utamaduni wa uadilifu ambao unastawisha uongozi wenye maono hata Katika mazingira ya migogoro", Dkt. Gwajima alisema panapo migogoro wanapaswa kuchukua kama fursa kwa maana katika kuchambua asili ya mgogoro huo watapata mfumo utakaozuia kutokea kwa mgogoro siyo huo tu bali na mingine mingi na taasisi itaenda mbele zaidi.

Katika Maadhimisho haya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatoa huduma ya kuwasikiliza  watumishi na wananchi kwenye viwanja vya ofisi zake zote  zilizopo jijini Dodoma pia itafanya usafi kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma pamoja na kuwatembelea wagonjwa Kwenye vituo vya kutolea huduma jijini hapa.

Waziri wa Afya Dkt.Dorothy Gwajima akiongea na watumishi wa Wizara ya Afya Kwenye viwanja vya wizara Kwenye mji wa Serikali Mtumba Kwenye Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Leonard Mchau akiongea wakati wa kikao hicho ambacho kilikuwa na lengo la kusikiliza changamoto za watumishi
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Idara Kuu Afya Bi.Deodatha Makani  akiwa Kwenye kikao hicho
Mmoja wa watumishi wa Wizara hiyo akichangia wakati wa kikao Cha Waziri wa Afya na watumishi wa Wizara hiyo ikiwa ni kutekeleza Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma

Baadhi ya watumishi waliojitokeza Kwenye kikao Cha Waziri Dkt.Gwajima wakifuatilia   wakati Waziri akiongea
Watumishi wa Idara Kuu Afya na Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Waziri wao wakati wa kikao Cha pamoja kilichofanyika Leo jijini Dodoma

 Picha ya pamoja ya Waziri Dkt.Gwajima akiwa na watumishi wa Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Mara baada ya kumalizia kikao hicho

Picha ya pamoja ya Waziri wa Afya,viongozi na baadhi ya watumishi wa Idara Kuu AfyaNa.Catherine Sungura,Dodoma

Viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wametakiwa kuwa

na utaratibu wa vikao kila baada ya miezi mitatu pamoja na mawaziri wao kwa lengo la kujadili mafanikio na changamoto na kuziwekea mpango wa pamoja wa kuzipatia majibu.

Rai hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima  wakati wa kikao chake na watumishi wa Idara mbili zilizopo Kwenye wizara yake(Afya na Maendeleo ya Jamii) Cha kusikiliza na kutatua changamoto zinazoikabili wizara hiyo zikiwemo za watumishi hao.

Mkutano huo ambao umefanyika Kwenye viwanja vya wizara hiyo zilizopo Kwenye mji wa Serikali Mtumba ikiwa ni Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza tarehe 18-23 Juni, 2021.

Dkt.Gwajima amesema anatamani kuona wizara hiyo inakuwa ya mfano wa katika kutambua na kuzipatia majibu changamoto zinazowakabili watumishi wake na wateja wake hivyo, amewataka wakurugenzi kuweka utaratibu wa kukutana kila baada ya miezi mitatu.

"Changamoto nyingi zinaweza kutatuliwa ndani na viongozi  yaani zipo ndani ya uwezo wetu kinachohitajika ni uratibu baina yetu, hivyo upo umuhimu wa kukaa pamoja kila baada ya miezi mitatu na kuongea na watumishi wetu kwa ajili ya kuchota mawazo na uzoefu".Alisisitiza

Hata hivyo  Dkt. Gwajima aliwataka watumishi hao kuwajibika na kuwa waadilifu wanapotekeleza majukumu yao na pia kutengeneza mfumo ambao utawajenga watumishi hao katika utumishi wenye viwango stahiki vya kitaifa na kimataifa.

Akielezea kaulimbiu ya mwaka huu inayosema "Kujenga Afrika tunayoitaka, kupitia utamaduni wa uadilifu ambao unastawisha uongozi wenye maono hata Katika mazingira ya migogoro", Dkt. Gwajima alisema panapo migogoro wanapaswa kuchukua kama fursa kwa maana katika kuchambua asili ya mgogoro huo watapata mfumo utakaozuia kutokea kwa mgogoro siyo huo tu bali na mingine mingi na taasisi itaenda mbele zaidi.

Katika Maadhimisho haya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatoa huduma ya kuwasikiliza  watumishi na wananchi kwenye viwanja vya ofisi zake zote  zilizopo jijini Dodoma pia itafanya usafi kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma pamoja na kuwatembelea wagonjwa Kwenye vituo vya kutolea huduma jijini hapa.

No comments :

Post a Comment