
Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati akifunga maonyesho
ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa
kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yaliyokuwa na lengo
kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi, yaliyomaliza leo Juni 2,2021 katika
uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma
Mjini,Mwalimu Josephat Maganga,akizungumza wakati wa kufunga maonyesho
ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa
kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yaliyomaliza leo Juni
2,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa
la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt .Adolf Rutayuga, akizungumza wakati waa
kuhitikishwa kwa maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi
yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi
(TPSF) kwa lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi,yaliyomalizika leo
Juni 2,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi
NACTE John Kondoro, akielezea jambo kwa washiriki wakati wa kuhitimishwa
kwa maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na
NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) kwa lengo
kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi,yaliyomalizika leo Juni 2,2021
katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Francis Nanai ,akizungumza wakati wa
kuhitimishwa kwa maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi
yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi
(TPSF) kwa lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi,yaliyomalizika leo
Juni 2,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Baadhi ya wanannchi waliohudhuria
Maonyesho hayo wakifatilia hotuba ya Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati akifunga
maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE
kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yaliyokuwa na lengo
kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi, yaliyomaliza leo Juni 2,2021 katika
uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi tuzo
ya pili ya elimu ya mafunzo na
ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta
binafsi (TPSF) yaliyokuwa na lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi,
yaliyomaliza leo Juni 2,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako,akipokea zawadi yake aliyopewa na
wanafunzi wa UDOM mara baada ya kufunga maonyesho ya pili ya elimu ya
mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya
sekta binafsi (TPSF) yaliyokuwa na lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya
ufundi, yaliyomaliza leo Juni 2,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
…………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ametoa wito kwa waajiri
nchini kutoa nafasi kwa wanafunzi wa vyuo vya ufundi kufanya mafunzo kwa
vitendo kwenye maeneo yao ya kazi ili kuwaandaa kabla hawajapata soko
la ajira
Wito huo ameutoa leo
Juni 2,2021 jijini Dodoma wakati akifunga Maonesho ya Pili ya Elimu ya
Mafunzo na Ufundi Prof.Ndalichako amesema kuwepo kwa ushirikiano
kutaondoa changamoto kubwa wanayokutana nayo wamiliki wa vyuo ya kupata
sehemu ya kuwezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo.
“Baadhi ya waajiri
wamekuwa na matazo hasi na kukukataa kuwapokea wanafunzi kwa madai kuwa
wanawapotezea muda kwa sababu wanaona kama bado hawajaiva hivyo naomba
muone umuhimu wa kuwapatia nafasi ya mafunzo kwa vitendo na kuwafanyia
tathimini kabla hawajamaliza .” Amesema Prof Ndalichako.
Amesema kupitia fursa
ambazo zinatolewa na waajiri kama kutakuwa na mapungufu kwa wanafunzi
wanaporudi vyuoni kabla ya kumaliza mafunzo yao vyuo vitachukua hatua za
kurekebisha na italeta manufaa zaidi kwa waajiri.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi
NACTE John Kondoro,amesema kuwa kufanyika kwa maonesho haya kunasaidia
kuchochea ustawi wa sekta ya elimu na mafunzo ya ufundi nchini na
yamewezesha wananchi kuona mchango mkubwa unaotolewa na vyuo vya ufundi
katika kuandaa raslimali watu itakayotumika katika ujenzi wa uchumi wa
viwanda.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mwalimu
Josephat Maganga ameziomba taasisi zinazotoa mikopo kuona namna ya
kutanua wigo wa kuwasaidia vijana wanaobuni vitu mbalimbali kuweza
kupata mitaji.
Awali Katibu Mtendaji wa Baraza la Vyuo vya
Ufundi Nchini (NACTE), Dkt.Adolf Rutayuga amesema kuwa maonyesho hayo
yamekuwa na mwitikio mkubwa kwani mwaka huu Taasisi 151 zimeshiriki
tofauti na mwaka 2019 ambapo Taasisi 139 zilishiriki.
Dkt.Rutayuga amesema kuwa takwimu inaonyesha
kuwa jumla ya wananachi waliotembelea mabanda imeonyesha kuongezeka
kutoka watu 14,500 mwaka 2019 hadi 14,730 mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Francis Nanai amesema sekta
Binafsi imekuwa ikitoa nafasi za mafunzo kwa vitendo na itaendelea
kupokea vijana wengi zaidi kujifunza kwa vitendo.
Aidha Nanai ameiomba
serikali kuanzisha chombo cha juu cha kuratibu suala zima la kukuza na
kuendeleza ujuzi nchini na pamoja na kulinda maslahi ya Taifa na ajira
za vijana wa kitanzania kuangalia upya masharti ya vibali vya ajira za
kazi.
Naye Mkuu wa Kitengo
cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam
(DIT) Amani Kakana,ambaye ni mshindi wa jumla wa maonyesho, amesema hawatabweteka katika ushindi huo na wataendelea kuongeza juhudi kutatua changamoto katika jamii.
Maonesho ya Pili ya
Elimu ya Mafunzo na Ufundi yamefanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini
Dodoma kuanzia Mei 27 hadi Juni 2, 2021 na yameshirikisha Taasisi 151.
Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni “Kuimarisha Ushirikiano na Wadau katika
Kukuza ujuzi kwa Maendeleo ya Viwanda”
No comments :
Post a Comment