Wednesday, June 9, 2021

WAZIRI LELA AIPONGEZA EQUITY BANK (T) KWA KUONGEZA UFANISI KATIKA UTALII ZANZIBAR

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Mh. Lela Mohamed Musa akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Equity Tanzania Robert Kiboti katika Mkutano wa Benki ya Equity kwa Wafanyabiashara wa Zanzibar jana


Akizingumza katika Semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Equity (T) Robert Kiboti amaesema kuwa Benki hiyo inajivunia kuwa mdau mkubwa wa malipo ya kidijitali visiwani humo kwa kuwa na Zaidi ya asilimia 60 ya mashine zote za malipo (POS) katika hoteli na vituo mbalimbali vya huduma Unguja na Pemba.

”Equity Bank inajivunia kuweza kutoa masuluhisho ya malipo kwa watalii na wenyeji wa Zanzibar ambapo Zaidi yam ashine za POS pia tunatoa huduma kupitia mawakala, huduma kupitia simu za mikononi na huduma kupitia mtandao wa Intaneti” alisema.




========   ========

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar Mh. Lela Mohamed Musa ameipongeza Benki ya Equity kwa kuongeza ufanisi katika utalii wa Zanzibar kupitia uwekezaji katika mifumo ya kiditali ya malipo na hivyo kurahisisha malipo ya utalii visiwani humo.

Akizungumza katika semina maalum iliyoandaliwa na Benki ya Equity kwa wafanyabiashara wa Zanzibar, Waziri Lela amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiri kuondokana na malipo ya fedha taslimu katika sekta ya utalii hivyo juhudi za Benki ya Equity kuweka mifumo anuai ya malipo ya kidijitali ina akisi juhudi hizo. 

“Sekta ya utalii ni mhimili mkubwa wa uchumi wa Zanzibar kwani inatoa  ajira, kuongeza pato la taifa na kuwa chanzo kikuu cha Fedha za kigeni. Mathalan, mwaka 2019, Zanzibar ilipokea takriban watalii laki tano na hivyo kuchangia karibu asilimia 28 za pato la ndani la taifa (GDP) huku ikichangia asilimia 82 ya fedha za kigeni. 
Hii inamaanisha kuwa utalii ni sekta muhimu sana kwetu, hivyo hatuna budi kuweka mazingira rafiki ya kufanya malipo kwa wageni wetu ili hatimaye watumie fedha nyingi Zaidi. Naipongeza sana Benki ya Equity kwa kuendelea kuwa wabunifu na ni matumaini yangu kuwa mkutano huu utakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha namna tunavyowahudumia wateja wetu na kuwapa nia mbalimbali za kufanya malipo yao. Serikali ina ahidi kuendelea kuweka mazingira rafiki ili kuongeza tija Zaidi kwenye utali” alisema.

Waziri Lela alisema pia kuwa Serikali ya awamu ya nane imedhamiria kuhakikisha kuwa mlipo na makusanyo yote yanafanyika kwa njia ya mtandao ili kuachana na mfumo wa kutumia pesa taslimu ambao umeonesha kuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuvutia wahalifu.

No comments :

Post a Comment