Wednesday, June 9, 2021

TTB YASHIRIKISHA WADAU WA UTALII KATIKAA KUBORESHA MKAKATI WA KUTANGAZA UTALII KUSINI MWA TANZANIA

Msimamizi wa Mradi wa REGROW upande wa TTB, Elirehema Maturo akitoa wasilisho wakati wa kogamano.

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Solimar Internatonal Limited ya Marekani, Chris Seek akiwasilisha mkakati mahususi wa kutangaza utalii kusini katika kongamano lililofanyika katika hotel ya Dar es Salaam Serena.

Wadau washiriki wa kongamano wakitoa maoni na mapendekezo yao kuhusiana na mkakati wa kutangaza utalii wa kusini.

Picha ya pamoja ya washiriki wa kongamano la makakati wa kutangaza utalii wa kusini mwa Tanzania.

……………………………………………………………………

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kupitia Mradi wa Kuendeleza Utalii wa Kusini (REGROW) imeandaa kongamano  la mkakati mahususi wa kutangaza utalii wa kusini mwa Tanzania. TTB imekusudia kuwajengea uwezo wadau wa utalii wa Dar es Salaam ili waweze kutumia mkakati

huo katika kutangaza na kuuza vifurushi vya utalii vya kusini.  Kongamano hilo la siku moja limefanyika leo tarehe 9/6/2021 katika hoteli ya Dar es Salaam Serena.

Katika kongamano hilo Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Solimar Intarnational Limited ya Marekani, Chris Seek amepata fursa ya kuwasilisha mpango mkakati na kupata mawazo ya wadau wa utalii kwa ajili ya maboresho ya mpango huo. Solimar ndiyo kampuni iliyopewa dhamana ya kutengeneza mpango mkakati huo pamoja na video mbalimbali zitakazotumika kutangaza utalii  wa kusini.

Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau wa utalii wa Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha na Morogoro. TTB imeandaa kongamano jingine ambalo linatarajia kufanyika mkoani Iringa tarehe 11/06/2021.

 

No comments :

Post a Comment