Na Karama Kenyunko Michuzi TV
WAFANYANIASHARA
14, waliokuwa wakituhumiwa kuwatumikisha walemavu na kuwafanya ombaomba
wamejikuta wakiangua kilio katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada
ya kusikia kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) hana nia ya
kuendelea na mashtaka dhidi yao hivyo wanaachiwa huru.
washtakiwa hao walionekana kama hawaamini kilichotokea na kubakia wakilia kwa uchungu.
Mapema,
wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu
Mkazi Mwandamizi Kassian Matembele kuwa kesi hiyo leo Juni 22, 2021
imekuja kwa ajili ya kutajwa lakini DPP amewasilisha hati ya
kutokuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao chini ya Kifungu Cha
91 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).
Washtakiwa
walioachiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kassian Matembele ni
Yusuph Mohamed (35), Yusuph Magadu (20), Emmanuel Salu (20) Gogad
Mayenga (18), Samson Taruse (26), Hussein John (18), Zacharia Paul (18),
Dotto Shigula (19), Petro Simon (21), Emmanuel Sahani (38), Joseph
Mathias (20), Masanja Paul (21), Aminiel Sangu (19), na Emmanuel
Lusinge.
Awali
washtakiwa hao walikuwa 15, lakini mshtakiwa wa kwanza ambae ni
mfanyabiashara Sadikiel Meta (71) aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka 41
yakiwemo ya kuwatumikisha walemavu na kuwafanya kuwa omba omba,
alifariki dunia na hiyo kubakia watuhumiwa 14.
Taarifa
ya kifo cha Meta, ilitolewa na Wakili wake, Robert Langeni, ambapo
alidai kuwa mteja wake alifariki Januari 28,2021 katika Hospitali ya
Temeke alipokuwa amelazwa.
Katika
kesi hiyo washtakiwaban walidaiwa wanashtakiwa walidaiwa kuwatumikisha
walemavu na kuwafanya kuwa omba omba, usafirishaji haramu wa binadamu,
kutakatisha fedha, kukwepa kulipa kodi na kuisababishia serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasara ya Sh. Milioni 31.3
Walidaiwa
kutenda kosa hilo kati ya mwaka 2020 na Januari Mosi 2021 jijini Dar es
Salaam ambapo kwa pamoja wanadaiwa kushiriki kufanya uhalifu wa kupanga
kwa kuongoza genge la uhalifu na kutekeleza kufanikisha kusafirisha
binadamu kwa haramu.
Pia
katika shtaka la usafirishaji haramu wa binadamu inadaiwa, katika
kipindi hicho hicho huko Tandale ndani ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar
es Salaam mshtakiwa Meta na Mohamed waliwatumikisha walemavu 37 na
kuwafanya wawe omba omba wa mtaani kwa lengo la kujipatia kipato.
Miongoni
mwa wa walemavu hao ni mtoto Kashinje Emmanuel, mwenye umri wa miaka
saba, Doto Silas Happines Bezagurwa, Neema Edward na Peter Sereke wote
wa ama umri wa miaka 11.
llidaiwa
kuwa washtakiwa hao pia walikuwa wakisafirisha walemavu kutoka mikoa ya
Shinyanga na Tabora kwenda Dar es Salaam na kwamba wakishapokelewa
wanawaingiza kwenye shughuli za omba omba kwa lengo la kujipatia faida.
No comments :
Post a Comment