Kaimu
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Mtahiko Henry (katikati)
akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuzungumzia tukio la
Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation kufanya
usafi maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni kuadhimisha
kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma.

Baadhi
ya Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation
wakizunguka kufanya usafi maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam
ikiwa ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma leo.
Sehemu
ya Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation
wakisafisha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni
kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma leo.
Gari
la Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation likiwa limejaa
taka zilizokusanywa na Watumishi wa Shirika hilo mara baada ya kufanya
usafi baadhi ya maeneo ya jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni kuadhimisha
kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma leo.
Baadhi
ya Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation
wakifanya usafi baadhi ya maeneo ya katikati ya jiji la Dar Es Salaam
ikiwa ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma leo.
Baadhi
ya Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania wakipakia uchafu kwenye
gari la TTCL walipokuwa wakifanya usafi baadhi ya maeneo ya jiji la Dar
Es Salaam ikiwa ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma
leo.
Baadhi
ya Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation
wakifanya usafi baadhi ya maeneo ya katikati ya jiji la Dar Es Salaam
ikiwa ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma leo.
Baadhi
ya Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation
wakifanya usafi baadhi ya maeneo ya katikati ya jiji la Dar Es Salaam
ikiwa ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma leo.
Na Mwandishi Wetu, Dar
WAKATI
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi kwa Umma yakifikia kilele chake leo
June 23, 2021 Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL
Corporation wamefanya usafi maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam
kitendo walichokiita 'Matembezi ya Usafi' ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
hayo.
Katika
matembezi hayo Watumishi wamepita katika maeneo ya Posta Mpya, IFM,
Soko la Kimataifa la Feri ambapo pamoja na mambo mengine walikuwa
wakiokota taka zote zilizotupwa katika maeneo tajwa na kuyakusanya kwa
ajili yakuyapeleka katika maeneo maalum ya kuhifadhi takataka.
Maadhimisho
haya ni kwa mujibu wa kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi
wanachama huadhimisha kwa kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu
Utumishi wa Umma yanaratibiwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora.
Akizungumzia
maadhimisho hayo Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw.
Mtahiko Henry amesema Wiki ya Utumishi wa Umma inamkumbusha kila
Mtumishi kwamba anawajibika kwa jamii na kumkumbusha kuwa utumishi wake
haupaswi kuishia Ofisini bali unaenda mbali zaidi kwa wananchi.
Aidha
Mtahiko amesema kupitia matembezi hayo Wananchi watapata fursa kuonana
na Watendaji wa TTCL uso kwa uso, na kupata maelezo mbalimbali ya huduma
na bidhaa zitolewazo na shirika hilo.
Pamoja
na kupata maelezo hayo wananchi pia watapata nafasi ya kutoa maoni
kuhusu huduma wanazozipata kutoka katika shirila lao la mawasiliano na
kwamba maoni yao yatathaminiwa kwakufanyiwa kazi kwakuhakikisha kero
itakayobainika inafanyiwa kazi.
“Sisi
ni Watumishi wa Umma kama walivyo watumishi wengine hivyo tunawajibika
kwa wananchi na ndiyo maana leo tumefanya shughuli ya kijamii ambapo
katika maeneo yote tulipopita tumeahakikisha tunayaacha mazingira yakiwa
safi.” Amesema Mtahiko
Ametoa
rai kwa Watumishi wote wa TTCL kuhakikisha wanaendelea kuzingatia
misingi ya utumishi wa Umma pindi wanapokuwa kazini na baada ya kazi
kutokana na ukweli kwamba jamii ndiyo inayowapima tabia na utendaji wao
wa kazi.
Katika
hatua nyingine Mtahiko amesema TTCL inawatumikia Wananchi
kwakuhakikisha inalipa kodi ya kila mwezi kwa wakati ambapo kupitia kodi
hizo mwananchi ananufaika kwakupata huduma mbalimbali za jamii ikiwemo
maji, barabara, elimu na Afya.
Wiki
ya Utumishi wa Umma Barani Afrika ni wiki maalum ya Watumishi wa Umma
na taasisi za Umma ambayo husherehekewa kuanzia tarehe 16 Juni hadi 23
Juni kila mwaka na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kwa lengo la
kutambua mchango wa Watumishi wa Umma katika maendeleo ya Bara la
Afrika.
Chimbuko
la Sherehe hizi ni uamuzi wa Mkutano wa Mawaziri wenye dhamana ya
Utumishi wa Umma uliofanyika Tangiers nchini Morocco mwaka 1994. Uamuzi
huu ulizitaka nchi za Afrika kusherehekea sherehe hizo kwa kauli mbiu
moja katika Bara zima la Afrika.
Malengo
ya msingi ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika ni pamoja na
kuwezesha watumishi wa Umma kutambua Dira, Dhima, na Malengo; Programu
na Mikakati; na Mafanikio na Changamoto zinazokabili Utumishi wa Umma,
kutambua mchango na umuhimu wa Watumishi wa Umma na umuhimu wao katika
kuleta maendeleo nyanja mbalimbali katika Taifa.
Lingine
ni kuhamasisha na kuwapa motisha Watumishi wa Umma ili waendelee na
kazi yao nzuri ya ujenzi wa Taifa na kuendelea kuwa wabunifu ili kutatua
changamoto mbalimbali katika jamii, Kupata mrejesho kutoka kwa wateja
na wadau wao juu ya huduma wanazozitoa na Kuwaandaa Watumishi wa Umma
ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali.
No comments :
Post a Comment