Wednesday, June 30, 2021

TFS YATOA MSAADA WA VITI, MEZA NA MADAWATI WILAYANI MUHEZA


Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo kushoto akipokea msaada wa madawati,viti na meza kutoka kwa Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga kwa ajili ya shule za Sekondari ,Msingi na Ofisi za Watendaji vyenye thamani ya Milioni 17.4 vilivyotolewa na Wakala wa Misitu Tanzania ( TFS)

Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo kushoto akipokea msaada wa madawati,viti na meza kutoka kwa Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga kwa ajili ya shule za Sekondari ,Msingi na Ofisi za Watendaji vyenye thamani ya Milioni 17.4 vilivyotolewa na Wakala wa Misitu Tanzania ( TFS)
MKUU wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo kulia akimkabidhi msaada huo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza mara baada ya kuvipokea kulia ni Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga
MKUU wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano iliyofanyika wilayani humo kulia ni Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga

Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano

Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano
Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Martha Chasama akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhianoMKUU wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo katika akiwa na Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga kulia akifuatiwa na Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Martha Chasama

Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika makabidhiano hayo

Sehemu ya madawati yaliyotolewa




NA OSCAR ASSENGA, MUHEZA

WAKALA wa Huduma za Misitu TFS shamba la Lunguza lililopo wilayani Muheza mkoani Tanga wametoa msaada wa madawati, viti na Meza vyenye thamani ya sh mil17. 4

Msaada huo ambao ni kwa ajili ya shule za msingi na Sekondari Tatu ambazo ni pamoja na Ofisi za watendaji kata mbili zilizopo wilayani Muheza utasaidia kuondosha changamoto zilizokuwepo awali.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo, Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga alisema kuwa msaada huo ni kwa ajili ya kusaidia kuboresha utoaji wa huduma.

"Tumetoa viti na Meza 17 kwa ajili ya Ofisi za watendaji na madawati 60 kwa shule za msingi na Sekondari" alisema Mwasalanga.

Awali akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo aliishuku TFS kwa namna walivyothamini elimu ya Watoto wa kitanzania na hivyo kwa msaada huo wataweza kuboresha utoaji wa elimu.

Mkuu huyo wa wilaya alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kuilinda misitu kuhakikisha hakuna uharibu unaofanyika.

"Niwaombe wananchi huu msitu unatunufaisha hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunaulinda ili uweze kutusaidia katika kukuza kipato chetu na uchumi" alisema DC Bulembo

Naye kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Martha Chasama alisema wametoa madawati 60 ambapo kati ya hiyo madawati 30 wametoa kwenye shule ya Msingi Kwemdimu, madawati 30 shule ya Sekondari Potwe na madawati 30 wametoa shule ya Sekondari Amani.

Alisema pia wametoa viti na meza 17 ambavyo wametoa ambapo thamani hizo ni sh.milioni 17.1 wao kama wahifadhi wanasema wahifadhi wa baadae ni watoto wadogo ambao wamewatolea thamani hizo.


“Misaada hiyo wanayoitoa kwa shule hizo na ofisi za watendaji tunaomba thamani hizo zitunzwe pamoja na walimu waangalia watoto namna wanavyocheza kwa sababu wakati mwengine wanaweza wakawa wanabonda madawati ili nao kama wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) waweze kupata nguvu ya kuendelea kutunzwa zaidi”Alisema

 

No comments :

Post a Comment