Viongozi
Mbalimbali wa bodi ya Maziwa na wanavikundi 14 wanaounda shirikisho la
wafugaji wa Ng'ombe wa Maziwa Kinondoni wakizindua shirikisho hilo leo
Mkoani Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa shirikisho la wafugaji wa Ng'ombe wa Maziwa wa Kinondoni wakiwa katika uzinduzi wa shirikisho lao leo.
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Dkt. George Msalya akizungumza wakati wa uzinduzi wa chama cha shirikisho la wafugaji wa ng'ombe wa Maziwa Kinondoni (UWANG'MAK) leo Mkoani Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa shirikisho la wafugaji wa ng'ombe wa Maziwa Kinondoni (UWANG'MAK) wakinywa maziwa wakati wa uzinduzi wa Chama cha Ushirika cha wafugaji wa ng'ombe wa Maziwa Kinondoni (UWANG'MAK) leo Mkoani Dar es Salaam.
CHAMA
cha Ushirika cha wafugaji wa ng'ombe wa Maziwa Kinondoni (UWANG'MAK)
imeiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwepo na vituo vya
kukusanya maziwa hapa nchini ili maziwa kuwa na viwango vya ubora.
Hayo
yamesemwa na mwakilishi wa wanachama cha ushirika wa wafugaji Ng'ombe
wa Maziwa wakati akiwasilisha Risala mbele ya Mgeni rasmi, Grace Ngassa
wakati wa uzinduzi wa chama cha ushirika cha wana UWANG'MAK leo Juni
30,2021 katika uzinduzi uliofanyika Mkoani Dar es Salaam. Amesema licha
ya kupata mafunzo katika maonesho ya nanenane lakini kunachangamoto ya
ukosefu wa Ng'ombe wa kisasa.
Licha
ya hayo wameomba kutengwa kwa maeneo maalumu kwaajili ya wafugaji wa
ng'ombe wa maziwa wa chama cha Ushirika cha wafugaji wa Ng'ombe wa
Maziwa Kinondoni (UWANG'MAK) ili waweze kufuga ufugaji wenye tija na
ufugaji wa biashara.
Mmoja
wa wanaushirika wa UWANG'MAK mesema kuwa ili kuwa na Ng'ombe wanaotoa
maziwa yenye ubora ni lazima Ng'ombe aweze kula majani ya kijani mengi
ili aweze kushiba na kutoa maziwa mengi.
Kwa
upande wake Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Dkt. George Msalya
Amesema kuwa wafugaji wa Ng'ombe wa Maziwa wanahitaji kuzalisha maziwa
mengi na yenye viwango ili kukidhi mahitaji wa watu kwani kila mwananchi
anatakiwa kunywa maziwa lita 200 kwa mwaka.
Licha
ya hayo amesema kuwa ni mhimu kutafuta soko la uuzaji wa maziwa kwani
mnunuaji mmoja mmoja sio soko la uhakika, hivyo mtu mmoja asipo nunua
italeta kharaha kwa mfugaji.
Amesema
pia ni mhimu kuwa na viwanda ili kusaidia maziwa yanayozalishwa na
wafugaji wa Ng'ombe wa maziwa kupata soko la uhakika na hivyo uchumi wa
mmoja mmoja kukua na hatimaye uchumi wa taifa.
Licha
ya hayo amewaomba wafugaji wa Ng'ombe wa maziwa wawe na Lugha moja
ambayo itawasaidia katika kujikuza katika sekta hiyo mhimu na yenye
utajiri mwingi wa Vitamini.
Kwa
upande wake Katibu Tawala wa Kindondoni, Stella Msofe amesema kuwa
wanahakikisha wanapata wanashirikisho la Wafugaji wa Ng'ombe wa maziwa
mazao wanayoyazalisha yawe bora na yanayokidhi vigezo vyote
"Kwa
hiyo sasa turejee kujenga shirika ambalo ni imara ili liweze kusonga
mbele kwaajili ya tasnia yetu ya maziwa. Amesema Stella
Chama
cha Ushirika cha wafugaji wa ng'ombe wa Maziwa Kinondoni (UWANG'AMAK)
Chama hicho kimeshirikisha vikundiva wafugaji Ng'ombe wa Maziwa 14
viliopo Kinondoni mkoani Dar es Salaam.
No comments :
Post a Comment