Tuesday, June 8, 2021

TFRA YAHAMASISHA WAWEKEZAJI KUWEKEZA KATIKA VIWANDA VYA MBOLEA


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini, (TFRA), Profesa Anthony Mshandete akizungumza na waandishi wa habari kuelezea maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Kilimo, Adolf Mkenda leo Juni 9, 2021 katika ni ofisi za Wizara ya Kilimo jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA Stephan Ngailo na kushoto ni Dkt. Asheria Kalala, Mkurugenzi Idara ya Udhibiti Ubora, TFRA.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini, (TFRA), Profesa Anthony Mshandete akizungumza na waandishi wa habari kuelezea maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Kilimo, Adolf Mkenda leo Juni 9, 2021 katika nm ofisi za Wizara ya Kilimo jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini, (TFRA), Stephan Ngailo akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano, kuelezea maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Kilimo, Adolf Mkenda leo Juni 9, 2021 katika ofisi za Wizara ya Kilimo jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeaswa kuhamasisha uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vya Mbolea nchini ili kufanikisha upatikanaji wa mbolea kwa wakati na bei nafuu na kupunguza kiasi cha fedha za kigeni zinazotumika kuagiza mbolea nje ya nchi.

Amehamasisha uwekezaji huo kwa sababu nchini hapa kuna miundombinu rafiki, upatikanaji rahisi wa malighafi na skko kubwa la mbolea ndani na njebya nchi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TFRA, Profesa Anthony Mshandete ameyasema hayo leo Juni 9, 2021 katika ofisi za Wizara ya kilimo jijjiji Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Kilimo, Adolf Mkenda.

Amesema, ni matumaini ya serikali kuwa juhudi hizo zitachangia upatikanaji wa mbolea bora kwa wakati na bei nafuu ili kuongeza tija katika uzalishaji, kuongeza kipato kwa mkulima, uhakika wa usalama wa chakula na kuchangia kwenye kukuza uchumi.

Aidha Profesa Mshandeta ameyataja maagizo waliyopewa na Waziri kuwa, waongeze muda wa kutangaza zabuni ili kupata washiriki wengi kutoka ndani na nje ya nchi na kuongez ushindani ili hatimae kuweze kupatikana bei shindani na nafuu kwa mkulima.

Pia wameagizwa kuanza mfumo wa kutangaza zabuni za uagizaji mbolea nchini katika balozi za nchi mbalimbali zinazozalisha mbolea duniani na kuendelea na utaratibu wa kutangaza zabuni za BPS kwa kutumia wazabuni walioko kwenye kanzidata ya mamlaka ili kuhakikisha mbolea zinawasili nchi kwa wakati wa msimu wa kilimo 2021/22.

"Kwa ujumla mahitaji ya mbolea nchini yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka, kwa mwaka 2017/2018 mahitaji yamekuwa tani 485,000 na mwaka 2020/2021 mahitaji yamekuwa tani 718,051,"amesema Mshandete.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA Stephan Ngailo
amesema kwa mwaka mamlaka hiyo inatumia zaidi ya Dola za Marekani milioni mbili na kwa tangu 2017 hadi 2021 imetumia trilioni 1.6.

Amesema asilimia 90 ya mbolea inaagizwa kutoka nje ya nchi na asilimia 10 ndio inatengenezwa hapa nchini na kwamba mbolea zinazozalishwa ni kwa ajili ya kupanda na kukuza mazao.

"Kuhamasisha uwekezaji ndani kutapunguza kiasi cha fedha za kigeni zinazotumika na badala yake zitatumika kwa kazi za maendeleo." amesema Ngailo.

Amesema kampuni zilizopo ni 13 za ndani na nje hivyo, wanatarajia kuongeza idadi kubwa zaidi kuleta ushindani ili mkulima apate mbolea kwa bei nafuu.

Wamehamasisha wawekezaji kujenga viwanda vya mbolea nchini kwani bado hamasa ni ndogo kuna kiwanda kimoja kutajengwa kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa ndani.

"Viwanda vidogo viongeze uzalishaji ili kutosheleza mahitaji ya nchi na baadae ziweze kuuzwa nchi jirani na kuleta fedha nying in za kigeni. Kampuni zote zikitengeneza mbolea ya kutosha italeta msaada kupata soko kubwa kwa sababu fursa zipo nyingi," amesisitiza.

 

No comments :

Post a Comment