Tuesday, June 1, 2021

TASUBA YAINGIA MAKUBALIANO NA CHUO CHA TAALUMA YA UREKEBISHAJI TANZANIA (TCTA)


Kaimu Mkuu wa Chuo Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo  (TaSUBa) Bw. Gabriel Kiiza na Mkuu wa Chuo TCTA, Kamishna Msaidizi wa Magereza Joe Gideon Matani wakionyesha makubaliano hayo katika hafla ya utuliaji saini kwa maafisa wa Magereza na TaSUBa (hawapo pichani). Wengine katika picha  (Kushoto) ni Mwanasheria wa TaSUBa, Daniel Awaki na (Kulia) ni Mkuu wa Mafunzo wa TCTA, SP. Mussa Goliama Mpandiko.
Baadhi ya maafisa wa Magereza  na TaSUBa wakifuatilia tukio la makubaliano katika hafla ya utuliaji saini kati ya TaSUBa na TCTA ya kuendesha mafunzo ya sanaa.
Picha meza kuu, maofisa wa tasuba na wakufunzi TCTA.
Kaimu Mkuu wa Chuo Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo  (TaSUBa) Bw. Gabriel Kiiza akizungumza katika hafla ya utuliaji saini makubaliano hayo. (Kushoto) ni Mwanasheria wa TaSUBa, Daniel Awaki na (Kulia) kwa Bw. Kiiza  ni Mkuu wa Chuo TCTA, Kamishna Msaidizi wa Magereza Joe Gideon Matani, akifuatiwa Mkuu wa Mafunzo wa TCTA, SP. Mussa Goliama Mpandiko.
Mkuu wa Chuo TCTA, Kamishna Msaidizi wa Magereza Joe Gideon Matani akizungumza katika hafla hiyo. (Kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Chuo TaSUBa, Bw. Gabriel Kiiza akifuatiwa na Mwanasheria wa TaSUBa, Daniel Awaki na (Kulia) ni Mkuu wa Mafunzo wa TCTA, SP. Mussa Goliama Mpandiko.
Kaimu Mkuu wa Chuo Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo  (TaSUBa) Bw. Gabriel Kiiza na Mkuu wa Chuo TCTA, Kamishna Msaidizi wa Magereza Joe Gideon Matani wakikabidhiana makubaliano hayo katika hafla ya utuliaji saini. (Kushoto) ni Mwanasheria wa TaSUBa, Daniel Awaki na (Kulia) ni Mkuu wa Mafunzo wa TCTA, SP. Mussa Goliama Mpandiko.

Na Mwandishi Wetu, DSM.

TAASISI ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeingia makubaliano ya

ushirikiano katika kuendesha Mafunzo ya Kozi za Sanaa na Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA).

Makubaliano hayo ambayo yamesainiwa leo Juni Mosi, katika hafla fupi iliyofanyika Chuo cha TCTA, Ukonga na wakuu wa Taasisi hizo mbili ambao ni Kaimu Mkuu wa Chuo TaSUBa Bw. Gabriel Kiiza na Mkuu wa Chuo TCTA, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Joe Gideon Matani wamekubaliana kwamba kwa pamoja wataandaa na kutoa mafunzo ya kozi za sanaa katika maeneo ya muziki, uigizaji na ngoma: pia mafunzo  yatakuwa yakitolewa kwa kipindi cha muda mfupi kisichopungua mwezi mmoja  na kisichozidi miezi mitatu kwa kila udhahili.

Awali kabla ya utiaji saini wa makubaliano hayo, Mkuu wa Chuo TCTA, Kamishna Msaidizi wa Magereza Joe Gideon Matani alisema kuwa, utiaji saini wa makubaliano hayo lilikua jambo la maandalizi la muda mrefu lakini sasa anafarijika kwa kuwa limekamilika na sasa kazi iendelee.

"Mashirikiano haya yatakua ni fursa nzuri ya kupeana uzoefu katika mafunzo ya Sanaa na Utamaduni kwa kuwa TaSUBa wamebobea na wana uzoefu katika utoaji wa mafunzo ya Sanaa na Utamaduni kwa miaka mingi. 

"Awali chuo chetu cha TCTA tulikuwa tunatoa mafunzo kwa Askari tu lakini sasa tumepanua wigo na tunatoa mafunzo kwa askari na raia." Alisema Mkuu wa Chuo hicho TCTA, Kamishna Msaidizi wa Magereza Joe Gideon Matani.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa TaSUBa, Bw. Gabriel Kiiza alisema, tasnia ya Sanaa na Utamaduni inahitaji ubunifu ili kuiboresha na kuleta vitu vipya kila wakati kuongeza ajira na kukuza uchumi katika Taifa.

"Tasnia ya sanaa na utamaduni ambapo mbali na kuwa ni burudani lakini sasa imekua ni sehemu ya ajira rasmi ambayo inahusisha kundi kubwa la vijana ambao ni nguvu kazi katika uchumi endelevu tunaamini ushirikiano huu utakuwa chachu kwa Taifa letu". Alisema Kaimu mkuu huyo wa TaSUBa, Bw. Gabriel Kiiza 

Bw. Kiiza aliongeza kuwa: 

TaSUBa ni miongoni mwa  Taasisi za Serikali zilizoanzishwa kwa ajili ya kutoa mafunzo ya sanaa, kufanya utafiti na kutoa ushauri katika maeneo ya sanaa na utamaduni.

"TaSUBa inadhamiria ya dhati ya kushirikiana na TCTA katika kuendesha mafunzo kwenye maeneo ya sanaa za muziki, uigizaji na ngoma". Alimalizia Bw. Gabriel Kiiza.

Katika makubaliano hayo waliotiliana saini, mafunzo yatatolewa na kuendeshwa katika madarasa ya TCTA ambapo maktaba pamoja na vifaa vya kujifunzia vitakuwa vya TCTA na endapo TCTA itakuwa na uhaba wa vifaa vya mafunzo, vitaazimwa kutoka TaSUBa kama vitakwepo vyakutosheleza. 

Vile vile, bila kuathiri Ibara ya 3(a) ya Makubaliano hayo, TCTA itakuwa na wajibu wa kuwasafirisha wanafunzi na kuwapeleka TaSUBa kabla ya kuhitimu mafunzo angalau mara moja kwa kila udhahili ili kuweza kujifunza mazingira ya TaSUBa. 

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ni Wakala wa Serikali ulioanzishwa chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ambapo Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania ni Taasisi halali ya Serikali chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

No comments :

Post a Comment