Kaimu Mkurugenzi Uwezeshaji na Uwajibikaji Joyce Komanya akizungumza na waandishi kuhusiana na ukiukaji wa Haki za Binadamu.
Kaimu
Mkurugenzi wa Uchechemuzi na Maboresho wa LHRC Joseph Oleshangay
akizungumza matokeo ukikaukaji yanayofanyika sehemu za Hifadhi.
*Yataka waliohusika wachukuliwe hatua
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV.
KITUO
cha Sheria na Haki za Bindam(LHRC)kimelaani matukio ya ukiukaji wa
haki za binadamu unaofanywa na Askari wa Mamlaka Usimamizi ya
Wanyamapori Tanzania (TAWA) huku hatua zikishindwa kuchukuliwa na
mamlaka husika kwa wale waliohusika kufanya ukiuaji huo.
Mauaji
yamekuwa yakifanywa kwenye hifadhi lakini kukiwa na mamlaka
kujichukulia hukumu ya kuua watu licha kuwepo kwa vyombo vya kutoa haki
dhidi ya wanaokiuka sharia zilizowekwa katika hifadhi hizo nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa
Kituo hicho Anna Henga kufuatia na tukio lililotokea hivi karibuni
mkoani Tabora kufuatia TAWA kwa kushirikiana na Askari Polisi wa Kituo
cha Polisi cha Igagala kuchoma nyumba kwa amri ya mkuu wa Wilaya ya
Kaliua aliyekuwepo katika kipindi cha hivi karibuni.
Henga
amesema kuwa katika nyumba iliyochomwa ulikuwa na mtoto wa miaka minne
(4) Nyanzobhe Mwandu ambaye alifariki kwa mauaji ya kikatili hayo bila
ya kuwa na hatia hiyo na kuuawa kwa katika hifadhi ni jambo
lisilokubalika wa nchi inayofuata misingi ya Haki na Utawala bora.
Mkurugenzi
Mtendaji huyo amesema vitendo hivyo vimekuwepo kwa muda mrefu dhidi ya
ukiuaji wa haki za binadamu katika hifadhi za maliasili pamoja na
kutofauta taratibu za kuundosha watu katika maeneo hayo ili kufanya
maisha ya wanyama yawe katika starehe.
“Wanannchi
wanaokuwepo na sharia zimewekwa wakiwa kaika maeneo hayo kuwa wamekiuka
taratibu za kuwaondosha zipo na kuweza kuwafikisha mahakamani lakini
suala la kuua watu wakiwa katika maeneo hayo halipo.” Amesema Henga.
Amesema aliyetoa amri kwa sasa hayupo lakini suala la jinai haliwezi likaisha hata miaka 1000.
Kifo
cha mtoto huyo zinasema kwamba serikali kupitia Mamlaka za Hifadhi ya
Taifa ilitenga eneo la Hifadhi katika Kijiji cha Ngitiri amabyo
inazunguka na Vijiji kadhaa Wananchi ambao mashamba yao yanapakana na
hifadhi hivyo walitakiwa waondoke ili kupisha ardhi iliyotengwa.
Taarifa
zinasema kuwa mwezi Januarie mwaka 2021 wananchi waliruhusiwa kulima
kwa makubaliano ya kwamba baada msimu wa mavuno kuisha walitakiwa
kuondoka katika eneo la mavuno.
No comments :
Post a Comment