Mkakati
mmoja wapo wa kukuza Uchumi wa nchi kupitia viwanda ni kuhakikisha
viwanda vinazalisha bidhaa ambazo zinakidhi matakwa ya viwango husika na
kufanya hivyo bidhaa zitapata masoko yawe ya ndani ama ya nje.
Ameyasema
hayo leo Meneja wa Mafunzo na Utafiti katika Shirika la Viwango
Tanzania (TBS), Mwl.Hamisi Mwanasala alipokuwa akizungumza na mwandishi
wetu katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam.
Aidha
Mwl.Mwanasala amesema kuwa viwango vinasaidia kutayarisha bidhaa iwe na
ubora na kukubarika katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
"Kiwango
ni muhimu katika kuona kwamba bidhaa inazalishwa iliyobora na salama na
kuwezesha kupata masoko na kukubarika na wateja wa bidhaa husika".
Amesema Mwl.Mwanasala.
Pamoja
na hayo Mwl.Mwanasala amesema kusudio la uwepo wa maadhimisho ya siku
ya viwango Afrika ni kwaajili ya kuenzi kazi kubwa iliyofanywa na wadau
mbalimbali wanaosimamia na kujishughulisha na masuala ya uendelezaji wa
viwango.
Shirika
la Viwango Afrika (ARSO) liliandaa mashindano Insha kwa wanafunzi wa
Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati ambapo Tanzania mashindano yanasimamiwa na
Shirika la Viwango Tanzania TBS, ikiwa Siku ya Maadhimisho ya Siku ya
Viwango Afrika Mei 6 mwaka huu washindi 10 watakabidhiwa zawadi na
watapelekwa kwenye mashindano ya Afrika kuiwakilisha Tanzania.
No comments :
Post a Comment