Mhandisi Idara ya
Uendeshaji wa UCSAF Shirikisho Mpanduji akiongea na waandishi wa habari
katika semina iliyotolewa na mkofuko huo kwa watoa huduma za mawasiliano
kanda ya Kaskazini.
Baadhi ya watoa huduma za mawasiliano kanda ya kaskazini wakisikiliza jambo katika semina waliyopewa na mfuko wa mawasiliano kwa wote(UCSAF) semina iliyofanyika mkoani Arusha.
*******************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Mfuko wa mawasiliano
kwa wote(UCSAF) uliyo chini ya wizara ya mawasiliano na teknolojia ya
habari umewajengea uelewa watoa huduma za mawasiliano kanda ya Kaskazini
kwa kueleza wajibu wa mfuko huo pamoja na wajibu wa watoa huduma hao
kwa mfuko.
Akiongea na waandishi
wa habari mhandisi Idara ya Uendeshaji wa UCSAF Shirikisho Mpanduji
alisema kuwa wajibu wa mfuko huo ni pamoja na kubainisha maeneo ya
miradi ya mawasiliano ambayo yanaweza kupata ruzuku kutoka katika mfuko
huo, kuweka vigezo vya maeneo ya utambuzi katika vijiji vinavyohitataji
na haviwezi kupata huduma ya mawasiliano kwa sababu ya kutokuwa na mvuto
wa kibiashara na kuanzisha mfumo madhubuti wa usimamizi wa fedha.
Alisema kuwa kazi
nyingine ya mfuko ni kuweka vigezo sahihi vya utoaji ruzuku kwajili ya
kupeleka huduma katika maeneo yaliyoainishwa, kufanya tafiti na
kufiatilia maendeleo ya mawasiliano maeneo ya vijijini na yale yasiyo na
mvuto wa kibiashara, kuishauri TCRA, kusimamia kisheria mikataba ya
utekelezaji wa majukumu ya ya utoaji huduma kwa wote pamoja na
kupendeleza sera madhubuti za mfuko kwa waziri wa sekta ya mawasiliano.
Aidha mhandishi
Shirikisho alieleza kuwa malengo ya mfuko huo ni kuhakikisha upatikanaji
wa huduma ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mjini
yenye mawasiliano hafifu, kuhamasisha sekta binafsi na serikali katika
utoaji wa huduma ya mawasiliano kwa wote, kuhamasisha maendeleo ya
kijamiina kiuchumi maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye
mawasiliano hafifu pamoja na kutengeneza mfumo kwaajili ya upatikanaji
wa mitandao ya mawasiliano na huduma rahisi zenye ufanisi katika
uzalishaji na upatikanaji wa soko la kiushindani.
“Lengo letu lingine
ni kuhamasisha utoaji wa huduma bora katika viwango nafuu na kuhakikisha
kuwa teknolojia ya habari na mawasiliano inapatikana vijijini na sehemu
za mjini zenye mawasiliano hafifu kwa bei nafuu,”Alisema Shirikisho.
Pia alisema kuwa hadi
sasa mfuko huo umetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya mawasiliano ya
simu za mkononi vijijini kwa kusaini mikataba ya kufikisha mawasiliano
katika kata 1057 zenye vijiji 3292 na wakazi 12,981,164 ambapo kata 705
zenye vijiji 2550 na wakazi zaidi ya milioni 8 tayari imeshakamika.
Alifafanua kuwa pia
mfuko umeweza kuanzisha vituo vya TEHAMA ambavyo vitaleta manufaa
makubwa kwa wananchi, mradi wa kuunganisha shule za serikali 711 na
mtandao wa internet pamoja na mradi wa wasichana na TEHAMA wa kutoa
mafunzo ya kuandika programu rahisi za kompyuta kwa wasichana 690 na
kuwashindanisha.
Kwa upande wao baadhi
ya washiriki wa mkutano huo akiwemo Odero Charles ambaye ni mmliki wa
watetezi Tv wanaishukuru mfuko huo kwani unatekeleza haki ya msingi ya
kupata na kutoa taarifa kwa kuzifikia sehemu ambazo hazifikiki ambapo
wao kama wadau wanataka mawasiliano yasiwe ya kutafuta kwa tochi.
Amos Ngosha mmiliki
kutoka voice of Afrika alisema kuwa kuna haja ya mfuko huo kuvitumia
vyombo vya habari kujitangaza ili wafahamike zaidi lakini pia kuionyesha
jamii fursa zilizopo katika mfuko huo.
Naye Maimuna Msangi
kutoka Pangani radio alisema kuwa wao kama wadau wana nafasi kubwa ya
kunufaika na mfuko huo kwa kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo
vitendea kazi ili jamii iweze kupata habari za kweli na uhakika.
No comments :
Post a Comment