Sunday, May 30, 2021

TAMOBA YAFANYA WASILISHO LA MFUMO MAALUM WA KIELEKTRONIKI WA ULINZI NA USALAMA WA BODABODA NA BAJAJI




Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TAMOBA, Joseph Kimisha, akibainisha faida za kiuchumi na kijamii za mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama kwa kuzuia na kudhibiti uhalifu unaotokana na vyombo vya moto hasa Pikipiki za miguu miwili na mitatu, Jijini Dodoma.



Kamishina wa Ushirikishwaji Jamii kutoka Makao Makuu ya Polisi Dkt. Mussa Ali Mussa akifuatilia wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama kwa kuzuia na kudhibiti uhalifu unaotokana na vyombo vya moto hasa Pikipiki za miguu miwili na mitatu, kutoka kwa Kampuni ya TAMOBA, Jijini Dodoma.



Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali (Ufuatiliaji), Devotha Gabriel akifuatilia wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama kwa kuzuia na kudhibiti uhalifu unaotokana na vyombo vya moto hasa Pikipiki za miguu miwili na mitatu, kutoka kwa Kampuni ya TAMOBA Jijini Dodoma, kulia kwake ni Afisa Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi na Idara hiyo, Ewald Bonifasi.



Baadhi ya wajumbe wa kikao wakifuatilia wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama kwa kuzuia na kudhibiti uhalifu unaotokana na vyombo vya moto hasa Pikipiki za miguu miwili na mitatu, kutoka kwa Kampuni ya TAMOBA Jijini Dodoma, Wajumbe hao ni kutoka Wizara ya Mambo ya ndani – Jeshi la Polisi, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mamlaka ya Serikali Mtandao pamoja na Ofisi ya WazirI Mkuu – Idara ya Uratibu wa Shughuli za serikali.





Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), Kaspar Kaspar Mmuya akifuatilia wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama kwa kuzuia na kudhibiti uhalifu unaotokana na vyombo vya moto hasa Pikipiki za miguu miwili na mitatu, kutoka kwa Kampuni ya TAMOBA, Jijini Dodoma.



…………………………………………………………..

Kampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaj Association (TAMOBA) imefanya wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama kwa kuzuia na kudhibiti uhalifu unaotokana na vyombo vya moto hasa Pikipiki za miguu miwili na mitatu.Lengo la wasilisho hilo ni kuutambulisha rasmi mfumo huo kwa Wizara, Idara na Taasisi za serikali.

Kwa mujibu wa wasilisho la TAMOBA,liliowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Joseph Kimisha, limebainisha kuwa zipo faida za kiuchumi na kijamii ikiwa ni pamoja na mfumo huo Kurahisisha udhibiti wa uhalifu kwa kupitia mfumo wa kielektroniki katika kupashana taarifa za wahalifu na kihalifu, Kukuza ajira kwa Vijana kwa kurasimisha biashara ya pikipiki (Bodaboda) na bajaji. Pia mfumo huo utaongeza ushirikishwaji wa jamii katika shughuli za polisi.

Kikao hicho kiliongozwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), Kaspar Kaspar Mmuya, na kuhudhuriwa na Wajumbe kutoka Wizara ya Mambo ya ndani – Jeshi la Polisi, Kamishina wa Ushirikishwaji Jamii kutoka Makao Makuu ya Polisi Dkt. Mussa Ali Mussa, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mamlaka ya Serikali Mtandao pamoja na Ofisi ya WazirI Mkuu – Idara ya Uratibu wa Shughuli za serikali.

Mfumo huo ulizinduliwa rasmi mwaka 2019 na aliyekuwa makamu wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ally Idd, jijini Dar es Salaam. Aidha, TAMOBA tayari wameandaa Kitabu cha Mwongozo wa kufichua na kuzuia Uhalifu kwa Polisi, Maafisa Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji ambapo wataanza na Usajili wa Pikipiki (Boda Boda) kwa kuanza na mkoa wa Dar es salaam kama mkoa wa majaribio, lengo likiwa ni kuifikia mikoa yote nchini.

Mnamo mwaka 1980 serikali iliruhusu kampuni binafsi za ulinzi kutoa huduma za ulinzi hapa nchini, chini ya uangalizi , uratibu na usimamizi wa Jeshi la polisi kwa mujibu wa Katiba na sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi wasaidizi kwa mujibu wa Sura ya 322, kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

 

No comments :

Post a Comment