Meya
wa Jiji la Dar es Salam Omari Kumbilamoto(katikati) akiwa na watendaji
wengine wa Jiji hilo pamoja na madiwani wa Kamati ya Fedha wakiangalia
mchoro wa jengo jipya la soko la Kisutu ambalo linatarajiwa kuanza
kutumika rasmi Mei 30 mwaka huu.
Ofisa
Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa Jiji la Dar es Salaam Tabu
Shaibu(wa pili kulia) akifafanua jambo wakati wa ziara ya madiwani wa
Kamati ya Fedha pamoja na watendaji wa Jiji hilo kufanya ziara ya
kutembelea soko hilo leo Mei 3,2021.
Meya
wa Jiji la Dar es Salaam Omari Kumbilamoto akifafanua jambo wakati
alipotembelea soko la Kisutu akiwa na wajumbe wa Kamati ya Fedha pamoja
na watendaji wa Jiji hilo.
Mmoja
wa maofisa wa Jiji la Dar es Salaa akielezea jambo kwa Meya wa Jiji
hilo pamoja na wajumbe wa Kamati ya Fedha baada ya kufanya ziara ya
kutembelea soko hilo.
Mhandisi
wa Jiji la Dar es Salaam John Magori akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu hatua mbalimbali za ujenzi zinazoendelea katika soko la Kisutu.
Wajumbe
wa Kamati ya Fedha wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa na Meya wa Jiji hilo
Omari Kumbilamoto baada ya kufanya ziara katika soko la Kisutu ambalo
linatarajiwa kuanza kutumika rasmi Mei 30 mwaka huu.
07:Meya
wa Jiji la Dar es Salaam akiwa na wajumbe wa Kamati ya Fedha wakipata
maelezo kuhusu ujenzi wa machinjio ya kisasa ya Vingunguti baada ya
kutembelea machinjio hayo.
Muonekano
wa nje wa jengo la Machinjio ya kisasa yaliyoko Vingunguti Jijini Dar
es Salaam ambapo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 97.
Meya
wa Jiji la Dar es Salaam Omari Kumbilamoto akijadiliana jambo na
maofisa wa Jiji hilo kabla ya kuanza kukagua ujenzi katika Machinjio ya
kisasa Vingunguti.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
SOKO
jipya la kisasa la Kisutu jijini Dar es Salaam linatarajiwa kuanza
kutumika rasmi Mei 30 mwaka huu ambapo zaidi ya wafanyabiashara 1500
watakuwa wakifanya biashara zao sokoni hapo.
Hayo
yamesemwa leo Mei 3,2021 na Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omari
Kumbilamboto baada ya Kamati ya Fedha kufanya ziara ya kukagua miradi ya
kimkakati inayoendelea kutekelezwa katika Jiji hilo ukiwemo mradi wa
soko hilo la kisasa la Kisutu pamoja na mradi wa ujenzi wa machinjio ya
kisasa Vingunguti.
kizungumzia
soko la Kisutu lenye ghorofa nne, Kumbilamoto amesema ujenzi wake
umegharimu Sh.bilioni 13.49 na ujenzi umefikia asilimia 97." Leo
tumefanya ziara ya kukagua miradi ya kimkakati iliyopo jijini Dar es
Salaam, miradi ambayo tumeitembelea ni mradi wa soko la Kisutu pamoja na
machinjio ya Vingunguti.
"Kwenye
soko hili la Kisutu ni matarajio yetu Mei 30 mwaka huu wafanyabiashara
waanze kufanya biashara zao hapa tutakuwa na wafanyabiashara wa aina
zote.Awali kabla ya ujenzi huu kulikuwa na wafanyabiashara 696 lakini
baada ya ujenzi huu litachukua wafanyabiashara 1500, hivyo hata mapato
ya Jiji la Dar es Salaam yataongezeka,"amesema.
Kwa
upande wa machinjio ya Vingunguti, Kumbilamoto amesema machinjio hayo
nayo yanatarajiwa kuanza kutumika mwishoni mwa mwezi huu na ujenzi
umekamilika kwa zaidi ya asilimia 96 na kiasi cha zaidi ya Sh.bilioni 12
zimetumika kujenga machinjio hayo.
Amefafanua
kabla ya ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa kwa siku zilikuwa
zinachinjwa ng'ombe kati ya 500 hadi 550 lakini baada ya ujenzi ya
ujenzi zitakuwa zinachinjwa ng'ombe 1500 na mbuzi 1000 , hivyo mapato
yatakuwa makubwa yatakuwa yakipatikana na hivyo kutatua changamoto
mbalimbali zilizopo.
"Lengo
na madhumuni yetu ni kukagua miradi yote ya kimkakati inayosimamiwa na
Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya CCM
ambayo tuliahidi kwa wananchi,"amesema Kumbilamoto.
No comments :
Post a Comment