Saturday, May 29, 2021

Shirika la SATF latoa sh milioni 51 kuimarisha utendaji

Afisa Mtendji Mkuu wa Shirika la Social Action Fund (SATF) linalojiusisha kusaidia kielimu kwa watoto walio katika mazingira magumu, Beatrice Mgaya, akizungumza na wadau watekelezaji miradi ya kusaidia watoto walio katika mazingira magumu (implementing partners) wakati wa kikao cha mpango kazi cha kuwa kawakabidhi kompyuta 18 yenye thamani ya shilingi milioni 51 mkoani Morogoro juzi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Social Action Fund (SATF) linalojiusisha kusaidia kielimu kwa watoto walio katika mazingira magumu, Beatrice Mgaya (kushoto) akiwakabidhi kompyuta na vifaa kuunganishia mtandao,Wawakilishi wa GSM Ruvuma, Paul Mwingira na Octovian Mnzava wakati wa mkutano wa mpango kazi na wadau watekelezaji (implementing partners) wa miradi ya kusaidia watoto walio katika mazingira magumu uliofanyika mkoani Morogoro juzi. Wa pili kushoto ni Mwakilishi wa Tamisemi, Dk. Johaness Balige na Meneja wa Miradi wa SATF, Nelson Rugambwa (kulia). 
Mwakilishi wa Tamisemi, Dk. Johaness Balige, akizungumza katika mkutano wa mpango kazi na wadau watekelezaji (implementing partners) wa miradi ya kusaidia watoto walio katika mazingira magumu uliofanyika mkoani Morogoro juzi wadau. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Social Action Fund (SATF) linalojiusisha kusaidia watoto walio katika mazingira magumu, Beatrice Mgaya (kushoto) akimkabidhi kompyuta na vifaa kuunganishia mtandao, Sista Suzana Misonji wa Kituo cha St. Maria Goreth kilichopo Bukoba mkoani Kagera wakati wa  kikao cha mpango kazi na wadau watekelezaji (implementing partners) wa miradi ya kusaidia watoto walio katika mazingira magumu uliofanyika mkoani Morogoro jana. Wa pili kushoto ni Mwakilishi wa Tamisemi, Dk. Johaness Balige na Meneja wa Miradi wa SATF, Nelson Rugambwa (kulia).
Wadau watekelezaji (implementing partners) wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Shirika la SATF wakati wa kikao cha mpango kazi.

======   =====   ======

Shirika la Social Action Fund (SATF) linalojihusisha na kuwawezesha kielimu

watoto walio katika mazingira magumu limekabidhi vitendea kazi vyenye thamani ya Sh milioni 51 zikiwemo kompyuta 18, ili kuimarisha utendaji kazi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika jana, mjini Morogoro, Meneja miradi wa shirika hilo, Nelson Rugambwa amesema vifaa hivyo vitasaidia katika utunzaji wa taarifa.

“Tumekabidhi vifaa hivi ikiwa ni pamoja na kompyuta 18 na vifaa vya kuunganishia mtandao vyenye thamani ya Sh milioni 51 kwa wadau watekelezaji (implementing Partners).

“Vifaa hivi vitasaidia katika utunzaji wa taarifa na kurahisisha mawasiliano ya kati yao na shirika, kwani tumeona katika kuboresha huduma zetu tuwapatie vitendea kazi wadau wetu ili kuwaondolea changamoto mbalimbali zilizokuwa zilizokuwa zikiwakwamisha katika utendaji wa kazi wao.

“Kwa sasa kazi zitakuwa rahisi maana watakuwa na kanzi data ya kutunza taarifa za miradi yao pamoja na kuwa na mawasiliano ya mtandao ya moja kwa moja na wasimamizi wa SATF kwa kufanya mawasiliano pasipo kulazimika kukutana,” amesema Rugambwa.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa (SATF), Beatrice Mgaya, mara baada ya kuwakabidhi vifaa hivyo  vyenye thamani ya Sh milioni 51 amewataka kufanya kazi kwa weledi na uaminifu.

“Tumetoa vifaa hivi kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi, hivyo tufanye kazi kwa kujitolea ili kusadia jamii hasa watoto, tuwawezeshe kupata elimu kutokana na changamoto zinazowakabili za ukatili, unyanyasaji, mazingira magumu na umasikini,” amesema.  

Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa wawakilishi wa vituo vya mikoa mbalimbali hapa nchini.

 

No comments :

Post a Comment