Wednesday, May 26, 2021

Serikali yatoa msaada Vifaa vya Uvuvi na Uchakataji Samaki kwa Chuo cha VETA Chato

Picha ya Pamoja ya Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako , Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke ,na Watendaji wa VETA mara baada ya makabidhiano ya Vifaa vya Uvuvi na Uchakataji Samaki kwa ajili ya Chuo Cha Ufundi Cha VETA Wilaya ya Chato. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt.Peter Maduki akizungumza kuhusiana na Vifaa vya Uvuvi na uchakataji Samaki vilivyotolewa na Serikali ya China ,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dkt.Pancras Bujulu akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Vifaa vya Uvuvi na Uchakataji Samaki ya Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Chato.
Balozi wa China Nchini Tanzania Wang Ke akizungumza kuhusiana  Vifaa vya Uvuvi na Uchakataji Samaki walivyotoa kwa ajili ya Chuo cha Ufundi Stadi VETA Wilaya ya Chato katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya VETA jijini Dar es Salaam.
Waziri Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza katika makabidhiano ya Vifaa vya Uvuvi na Uchakataji wa Samaki vilivyotolewa na Serikali ya China katika hafla iliyofanyika Makao Makuu VETA jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dkt. Pancras Bujulu akitoa maelezo  kwa Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Balozi wa China Wang Ke kuhusiana na  Vifaa vya Uvuvi na Uchakataji Samaki vilivyotolewa na Serikali ya China kwa ajili Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya Chato katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya VETA jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dkt. Pancras Bujulu akitoa maelezo  kwa Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Balozi wa China Wang Ke kuhusiana na  Vifaa vya Uvuvi na Uchakataji Samaki vilivyotolewa na Serikali ya China kwa ajili Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya Chato katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya VETA jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia  Profesa Joyce Ndalichako aikibadilisha hati  na Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke ya makabidhiano ya Vifaa vya Uvuvi na Uchakataji kwa Chuo cha Ufundi Stadi VETA cha Wilaya ya Chato katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya VETA jijini Dar es Salaam.

*Profesa Ndalichako aitaka VETA kutunza Vifaa hivyo 

Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa serikali inaendelea kuboresha vyuo vya ufundi stadi katika kuhakikisha vijana na wanapata ujuzi ulio bora pamoja na kuweza kuchangia maendeleo ya uchumi nchini.
 
Profesa Ndalichako amesema hayo Dar es Salaam leo Mei  wakati akipokea msaada wa vifaa vya mafunzo ya uvuvi na uchakataji wa mazao ya samaki vilivyotolewa serikali ya China kwaajili ya Chuo cha Veta, Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuvikagua na kuvipokea, Profesa Ndalichako, amesema vifaa vilivyotolewa ni majokofu, mashine za kusindika samaki, kutengeneza soseji za samaki na boti ya uvuvi vyenye  thamani yake ni Sh. milioni 350.

“Serikali ya Tanzania inaishukuru  Serikali ya China kwa msaada huu ambao ni mwendelezo wa urafiki na undugu wetu wa siku nyingi na mshirika katika maendeleo na kuutaka   uongozi wa VETA ukavisimamie  vifaa hivyo  ili vidumu”, alisema Profesa Ndalichako.

Ameesema kuanzisha kwa somo la Uvuvi na  uchakataji wa mazao ya uvuvi ili kusaidia wananchi wanaozunguka sehemu za Maziwa na Mito pamoja na bahari kuingia soma kozi hiyo ili kufanya Uvuvi wa Kisasa pamoja na watanzania wote.

Profesa Ndalichako  amesema  wananchi wa Chato, Kagera na mikoa ambayo wananchi wake wanategemea uvuvi kuinua kipato chao.

Aidha amesema watatekeleza ahadi zote walizozitoa kwenye Vyuo vya Ufundi Stadi VETA ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Hayati Rais John Magufuli.


“Hii Kozi  nataka sasa Veta mkalifundishe kwenye mikoa yenye maziwa kama kule kwetu Kigoma kuna Ziwa Tanganyika... hii itaboresha uchumi wa wananchi wa maeneo hayo.

Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke amewapongeza watanzania kwa kuwa na rasilimali nyingi huku akiahidi kuendelea kushirikiana na VETA katika kusukuma mbele  ujuzi kwa vijana ili waweze kuzalisha kwa tija .

“Niwatakie heri ya siku ya Afrika... Serikali ya China inafurahishwa na juhudi zenu za kuwekeza kwenye ujuzi. Tutaendelea kushirikiana ili kuleta maendeleo ya Tanzania na Afrika,” amesema Balozi Ke.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Dkt. Pancras Bujulu amesema mchakato wa upatikanaji wa vifaa hivyo ulianza Januari 6.2021 baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China alipotemebelea Tanzania na kuzindua rasmi Chuo cha Veta wilayani Chato.

 

No comments :

Post a Comment