Na Woinde Shizza ,michuzi Tv ARUSHA
WANANCHI
wanapaswa kuanza kufanya kilimo na ufugaji wenye tija. Namna bora ya
kukabiliana na changamoto za wafugaji na wakulima ni kutafuta mbinu
shirikishi zitakazohusisha wadau katika utatuzi, ili kuendelea kuongeza
uzalishaji. Wadau wa kilimo na ufugaji wanahitaji kuunganisha nguvu
kwa pamoja badala ya kumuachia mkulima na mfugaji kuhangaika na utatuzi
mwenyewe.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda katika ziara ya
siku ya pili kutembelea wakulima na wafugaji katika kijiji cha
Chemchem, kujionea miradi ya shirika lisilo la serikali la Food for his
children linavyosaidia kuimarisha familia duni kuweza kujikwamua
kiuchumi.
Amepongeza
jitihada zinazofanywa na shirika hilo kwa wananchi wa Karatu, hasa kwa
mafanikio ya dhahiri yaliyojikita katika ufugaji wa mbuzi wa kisasa aina
ya sane. Lakini kwa namna wananchi walivyopokea miradi hiyo na kuona
kama ni miradi ambayo inagusa maisha yao.
amesema
changamoto kubwa ya ufugaji wa kisasa ni malisho ya mifugo ambayo kama
ikitatuliwa itamsaidia mfugaji kupata maziwa kwa wingi.
Ametoa
rai kwa shirika la Food for his children kuona namna ya kuja na mbinu
shirikishi ili kumkwamua mfugaji hasa katika adha ya kupata malisho ya
mifugo.
Amesema
kama mbuzi mmoja wa kisasa kwa makadirio ya juu akitunzwa vizuri
anaweza kutoa lita tano kwa siku kwa maana ya kukamuliwa mara mbili
asubuhi na jioni. Basi ipo haja ya shirika kukaa na wafugaji ili kuja na
ufumbuzi wa changamoto zao kwa pamoja ili mwananchi aweze kunufaika
zaidia na ufugaji.
Mh.
Kayanda ameshauri shirika la Food for his children kupata takwimu
sahihi za wananchi waliojihusisha na mradi huo. Amesema kupata takwimu
za namna mbuzi wanavyozaliana lakini pia kupata takwimu za kiasi cha
mbuzi waliouzwa.
Amesema
takwimu ndio ziatakazosaidia kujua mafanikio ya mradi na udhaifu wa
mradi. Ameongeza kusema kuwa katika taarifa zao ni vyema wakawa na
wasifu za mfugaji mmoja mmoja lengo likiwa ni kufahamu matokeo ya mradi
kwa ujumla na matokeo ya mradi kwa mwananchi mmoja mmoja.
Meneja
wa mradi Bi, Honorina Honorati amesema mbuzi wa kisasa wanaosambazwa na
shirika la Food for his children, wanatabia ya kuzaa mapacha isipokuwa
tu kwa uzazi wa kwanza. Ameongeza kusema mbuzi hao wanaweza kuzaa mara
mbili kwa mwaka hivyo kumfanya mfugaji kuongeza idadi ya mbuzi lakini
kufaidika na maziwa ya mbuzi.
Bi,
Honorati amesema wafugaji wengi wa mbuzi wananufaika kwa biashara ya
kuuza mabeberu ambao wanauza mpaka kiasi cha shilingi 200,000 kulingana
na ukubwa na uzito. Amesema matarajio ya mradi ni kuona watu wengi
wanafanikiwa, na wanapenda kujihusisha kaitika ufugaji wa mbuzi wa
kisasa. Ili kutoa fursa kwa watu wengine wasioujua mradi kufundishwa na
kuelewa misingi ya mradi.
Mama
fabiola, Mfugaji wa mbuzi wa kisasa katika kijij cha Chemchem amesema
kitu kinacholeta faraja katika mradi huo ni upatikanaji wa maziwa ambao
unawawezesha kupata kipatao. Amesema katika miradi yake ya ujenzi
hutegemea kuuza mabeberu ambao wamekuwa na soko kubwa. Amesema katika
kijiji Chemchem changamoto kubwa wanayopata wafugaji ni fisi ambao
wananyemelea mifugo yao wakati wa usiku.
No comments :
Post a Comment