Wednesday, May 5, 2021

SERIKALI YAONDOA TOZO YA ASILIMIA SITA, YAFUTA TOZO YA ADHABU HESLB


Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imesema kuwa kuanzia mwaka mpya wa fedha unaoanza Julai 1, mwaka huu wa 2021 itaondoa rasmi tozo ya asilimia sita ambayo imekua

ikitozwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB.)

Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako wakati alipokua akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2021/22.

Kuondolewa kwa tozo hiyo na Wizara ya Elimu kupitia kwa Waziri Prof Ndalichako ni utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan siku ya Wafanyakazi Mei Mosi ambapo aliagiza kubakia kwa  tozo ya asilimia 15 inayokatwa kwenye mshahara kila mwezi na hiyo ya Asilimia sita iondolewe.

Prof Ndalichako amesema katika kulinda thamani ya Fedha katika urejeshaji wa mkopo kuanzia julai mosi 2021 basi tozo ya asilimia sita itaondolewa rasmi kwa wanufaika.

" Pamoja na kuondoa tozo hiyo ya asilimia sita pia naiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kuondoa tozo ya adhabu ya asilimia 10 ya mkopo ambayo imekua ikitozwa kwa wanufaika wanaochelewesha mikopo yao," Amesema Prof Ndalichako.

 

No comments :

Post a Comment