Kwa
niaba ya mshindi wa kwanza wa gari aina ya Tata Ace kwenye kampeni ya
Bonge la Mpango - Hadija Idd Mkazi wa Chamwino mkoani Dodoma, ambaye
ndiye mshindi wa kwanza kujishindia zawadi ya gari aina ya Tata Ace
kwenye kampeni hii - Jacqline Kihongozi akifungua gari hilo(Lifan) baada
ya kukabidhiwa na Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB-Benedicto
Baragomwa katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Tawi la NMB
Chamwino. Akishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati- Nsolo Mlozi.
Kadi:
Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB-Benedicto Baragomwa
akimkabidhi kadi ya gari aina ya Tata Lifan alimaarufu Kirikuu ,Jacqline
Kihongozi, aliyepokea kwa niaba ya mshindi wa kampeni ya bonge la
Mpango inayoendeshwa na NMB, Hadija Idd Mkazi wa Chamwino mkoani Dodoma
ambaye ndiye mshindi wa kwanza kujishindia zawadi ya gari aina ya Tata
Ace kwenye kampeni hii. Akishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati-
Nsolo Mlozi.
Hadija
Iddi mkazi wa Chamwino mkoani Dodoma amekuwa mshindi wa kwanza
kuzawadiwa gari aina ya TATA Ace maarufu kama Kirikuu yenye thamani ya
sh. Millioni 25, baada ya kushinda katika kampeni ya Bonge la Mpango
inayoendeshwa na Benki ya NMB.
Akimkabidhi
gari hiyo Bi. Hadija, Kaimu Afisa Mkuu Ukaguzi wa Ndani wa NMB,
Benedicto Baragomwa alisema, Bonge la Mpango inaendelea nchini kote na
zawadi mbakimbali zinaendelea kutolewa, hivyo wateja wanaendelee
kufungua akaunti na kuweka hela kuanzia sh. 100,000 kwenye akaunti zao
za NMB ili waweze kuingia katika kinyanganyiro cha Zawadi mbalimbali
zinazotolewa katika kampeni hii ikiwemo, gari ya kifahari aina ya Toyota
Fortuner mpya yenye thamani ya Sh.169 milioni, gari ya miguu
mitatu(Lifan) na pesa taslimu.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa gari hilo, Hadija aliishukuru benki ya NMB na
kusema kuwa gari hilo litamsaidia katika shughuli zake za kujiongezea
kipato lakini pia akawashauri watanzania kuwekeza katika benki hiyo
kwani ndiyo benki bora Tanzania na pia inawajali wateja wake kwani
amekuwa shahidi.
"Nimeamini
kuwa yanayozungumzwa ni kweli,nimekabidhiwa gari mpya,nimepewa ufunguo
na Kadi ya gari vikiwa kamili kabisa, kweli NMB ndiyo mpango
mzima,"alisema Hadija.
Wakati
huo huo, Meneja wa NMB Kanda ya Kati - Nsolo Mlozi na mwakilishi kutoka
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania walichezesha droo nyingine kwa
ajili ya kuwapata washindi wa wiki, ambapo watu mbalimbali walipata
fedha taslimu wakati na Henry Semwanza kutoka Chamwino and Faustine
Nyawigrika wa Biharamulo wakijishindia gari ya mataili matatu (Lifan)
mpya kila mmoja.


No comments :
Post a Comment