Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga (katikati)
akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Bi. Khadija Khamis Rajab alipotembelea Ofisi hiyo akiwa na Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mohammed Khamis Abdulla (kushoto).
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga akiwa na Naibu
Katibu Mkuu Ofisi hiyo Bw. Mohammed Khamis Abdulla wakiagana na viongozi
wa Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC) walipotembelea Ofisi hiyo Zanzibar.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (wa pili kulia)
akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili (Sera, Uratibu na
Baraza la Wawakilishi) Dkt. Khalid Salum Mohamed alipokutana naye katika
ukumbi wa wageni uliopo katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Wengine pichani kuanzia kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Bw. Mohammed Khamis Abdulla, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili
wa Rais Bw. Thabit Idarus Faina na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga akizungumza na
watumishi wa Ofisi hiyo katika Ofisi ya Zanzibar alipofanya ziara akiwa
na Naibu Katibu Mkuu Bw. Mohammed Khamis Abdulla.
Kuanzia
kushoto Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga
akiwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi hiyo Bw. Mohammed Khamis Abdulla,
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la
Wawakilishi) Zanzibar Bw. Thabit Idarus Faina na Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu Bw. Tixon Nzunda wakibadilishana mawazo katika viwanja vya
Baraza la Wawakilishi wakati wa ziara yao.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga akiwa na viongozi wengine na wadau wa mazingira kutoka sekta binafsi walipotembelea mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi eneo la Kilimani Mkoa wa Mjini Magharibi.
No comments :
Post a Comment