Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, anayeshughulikia
Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. James Mdoe akipata maelezo
kutoka kwa Naibu Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Dkt Prosper Mgaya
kuhusu mfumo wa taa za kuongozea Treni na magari uliobuniwa na
mwanafunzi wa chuo hicho. Dkt Mdoe alitembelea banda hilo wakati wa
Maonesho ya Pili ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi leo kwenye Uwanja wa
Jamhuri jijini Dodoma. Maonesho hayo yameandaliwa na Baraza la Elimu ya
Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania
(TPSF).
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Mdoe akitia
saini kwenye kitabu cha wageni katika Banda la Nacte kabla ya kuanza
kutembelea maonesho hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Nacte, Profesa
Kondoro.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Mdoe
(kulia) akitembelea banda la Chuo cha Taifa cha Utalii wakati wa
maonesho hayo.
Dkt.
Mdoe akipata maelezo kutoka kwa Meneja Msaidizi wa Mipango ya Muda
Mfupi wa Benki Kuu (BoT), Tulla Mwigune kuhusu alama mbalimbali muhimu
zilizomo kwenye noti alipotembelea banda hilo.
Dkt. Mdoe akitembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza NACTE, Profesa Kondoro.
Meneja
wa Kanda wa Kampuni ya Tera Technologies and Eng. Ltd. Christina
Enrisha akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia, Dkt. Mdoe kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na
kampuni hiyo ikiwemo mifumo ya ulinzi ya kielektroniki kama vile CCTV.
Dkt.
Mdoe akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Intermech
Engineering Limited, Injinia Peter Chisawillo kuhusu mashine mbalimbali
wanazozitengeneza za kuchakata mazao ya kilimo.
Mkurugenzi Ukuzaji Mitaala na Upimaji wa NACTE, Dkt.Annastellah Sigwejo (kushoto) akiangalia kifaa maalumu cha kufugia samaki.
Dkt. Mdoe akiangalia mashine iliyobuniwa ya kupepeta mazao.
Dkt.
Mdoe akizungumza kwa kutaka ufafanuzi alipotembelea Banda la Sugeco
ambalo moja ya kazi zake kuwafanyia atamizi vijana kwa kuwatafutia
masoko ya mazao wanayozalisha pamoja na kutengeneza vitalu nyumba vya
kukausha mazao.Kushoto ni Mwatamizi wa Sugeco, Fatuma Mbaga.
Mwenyekiti
wa Kikundi cha Kemmy Product, Penina Kaminyonge (kushoto) akimueleza
Dkt. Mdoe kuhusu bidhaa zao mbalimbali wanavyosindika ambazo wanauza
kwenye maonesho hayo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt James Mdoe
ametembelea Maonesho ya Pili ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwenye Uwanja
wa Jamhuri jijini Dodoma, ambapo amewapongeza wabunifu wa aina
mbalimbali walioshiriki katika maonesho hayo ambapo ameshangazwa na
msichana wa Chuo Kikuu cha St. Joseph ambaye amebuni kifaa kinachotoa
taarifa sehemu ivujayo gesi kwenye bomba.
Mdau,
nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Naibu Katibu
Mkuu akizungumza baada ya kutembelea maonesho hayo, Mkurunzi wa Kampuni
ya Intermech Engineering Limited, Injinia Peter Chisawillo akielezea
ubunifu wa mashine mbalimbali za kusindika na kuchakata bidhaa za mazao
mbalimbali lakini pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Ensol akielezea umuhimu
wa wanafunzi wawapo shule kuzingatia masomo na mambo mengine kuhusu
vifaa vya ulinzi vinavyotengenezwa na kampuni hiyo....
No comments :
Post a Comment