Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na wanufaika na wananchi wa
Kijiji cha Nyashigwe, Wilayani Magu mkoani Mwanza wakati wa ziara yake
ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kuhimiza
uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma mkoani Mwanza.
Baadhi
ya Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wananchi wa Kijiji
cha Nyashigwe wilayani Magu Mkoani Mwanza wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa
ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na
kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma mkoani Mwanza.
Afisa
Mtendaji wa Kijiji cha Nyashigwe, Bi. Devotha Aloys akiwasilisha
taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ya Kijiji
hicho kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa ziara ya kikazi ya
Waziri huyo ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kuhimiza
uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma mkoani Mwanza.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella akitoa neno la utangulizi kabla
ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa kukagua utekelezaji wa
miradi ya TASAF katika Kijiji cha Nyashigwe wilayani Magu.
Mnufaika
wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Nyashigwe wilayani
Magu, Bibi Marynsiana Tabu akitoa ushuhuda wa mafanikio aliyoyapata
kupitia ruzuku ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo ya kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa (aliyevaa tai) akielekea kushuhudia
mafanikio waliyoyapata wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
Kijiji cha Nyashigwe wilayani Magu, wakati wa ziara yake ya kikazi ya
kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Kijiji hicho. Wa kwanza
kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe. Salum Kalli.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akifurahia mafanikio aliyoyapata mnufaika
wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Kijiji cha Nyashigwe wilayani Magu,
Bw. Fabian Mtilanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Kijiji hicho.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa amewataka Watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia zoezi la
utambuzi na uandikishaji wa kaya maskini nchini kuwa waadilifu katika
kuziandikisha kaya zinazokidhi vigezo vya kunufaika na ruzuku inayotolewa na
Serikali kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini.
Mhe.
Mchengerwa ametoa onyo hilo kwa Watendaji hao akiwa katika ziara ya kikazi ya
kukagua utekelezaji wa mpango wa TASAF wilayani Magu mkoani Mwanza.
Mhe.
Mchengerwa amewahimiza Watendaji hao kuongeza umakini katika utambuzi ili zipatikane
kaya maskini zinazostahili kupata ruzuku.
“Ikibainika
kuna kaya zisizostahili kunufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, hatua kali
za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya waliohusika.” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Ameongeza
kuwa, Serikali imedhamiria kuzifikia kaya zote maskini nchini ili kuziwezesha
kaya hizo kuboresha maisha yao kwani lengo ni kuzikwamua kutoka katika lindi la
umasikini.
Aidha,
Mhe. Mchengerwa amewataka wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kutumia
ruzuku kwa kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo kama Serikali ilivyokusudia.
Ili
kuwawezesha wanufaika kutumia vema ruzuku wanayoipata, amewataka Maafisa Ugani wote
nchini kuwapa ushauri wa kitaalam wanufaika ili waweze kupata mavuno bora
yatakayotokana na ufugaji na kilimo cha kisasa.
Mhe.
Mchengerwa amehitimisha ziara yake ya kikazi Mkoani Mwanza iliyolenga kutatua
changamoto za Watumishi wa Umma, kuhimiza uwajibikaji na kukagua utekelezaji wa
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
No comments :
Post a Comment