Msimamizi
wa Uchaguzi Jimbo la Buhigwe Marycelina Mbehoma akikabidhi Cheti cha
ushindi mshindi wa kiti cha Ubunge Jimbo la Buhigwe Mkoani Kigoma,
Kavejuru Felix wa Chama cha Mapinduzi baada ya kuibuka mshindi na
kuwabwaga wapinzani wake 12 alioshiriki nao katika Uchaguzi mdogo
uliofanyika Mei 16,2021. Mgombea huyo alipata kura 25,274 Kati ya kura
30,320 ya kura halali zilizopigwa.
Mgombea wa ACT Wazalendo
Garula Kudra alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 4,749 na nafasi ya
tatu ikienda kwa Abdallah Bukuku wa Chama cha CHAUMA aliyepata kura 125.
No comments :
Post a Comment