
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Muhambwe, Bw. Diocles Rutema amemkabidhi cheti cha ushindi aliyekuwa Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo, Dkt. Florence Samizi.
Dkt.
Samizi ameshinda uchaguzi huo baada ya kupata kura 23,44I kati ya kura
35,339 sawa na asilimia 68 akifuatiwa na Mgombea wa Alliance for Change
and Transparency (ACT-Wazalendo), Bw. Masabo Julius aliyepata kura
10,847 na Mgombea wa Democratic Party (DP), Bw. Philipo Fumbo aliyepata
kura 368.
No comments :
Post a Comment