Na Woinde Shizza , michuzi Tv ARUSHA
Kutokana
na tatizo la kutokuwepo kwa ajira nyingi za moja kwa moja za
serikalini , wanafunzi wa vyuo vikuu wametakiwa kujiongeza na kuwa na
kitu cha ziada Cha kufanya nje na taaluma
Hayo yamebainishwa na
mkurugenzi wa Phide Intertaiment &tours ambaye pia ni muandaaji wa
Tuzo za wanawake na wanaume zijulikanazo kwa jina la Extraordinary men
awards 2021 pamoja Mwanamke Tuzo 2021 ,Phidencia Mwakitalima alipokuwa
akiongea katika uzinduzi rasmi wa Tuzo hizo za wanaume pamoja na ugawaji
wa zawadi ya Tuzo ya mwanamke uliofanyika jijini hapa.
Alisema
kuwa kumekuwa na tatizo kubwa la ajira za serikalini na hata
binafsi,wanafunzi wengi wamekuwa wakisoma lakini baada ya kumaliza
wanaenda kukaa tu mtaani bila ya kazi yeyote na hii inatoka na kukosa
ajira na ujuzi wa vitendo.
Aliwataka wanaume na wanawake kufanya
kazi kwa bidii bila kukata tamaa huku wakiamini kwamba kuna watu wengine
huko nje wanatambua mchango wao.
Alisema kuwa tuzo hizi
zitasaidia kuwapa motisha wanawake wajasiriamali ,wanaume pamoja na
wanafunzi kufanya kazi kwa bidii ,kwani inawasaidia pia kujitangaza
,pamoja na kuwa wamoja pamoja na kuwakutanisha na watu
mbalimbali,kujifunza mambo mbalimbali haswa katika biashara zao bila
kuangalia matatizo ambayo wanakabiliana nayo.
"Tuzo
hizi tumezigawa Katika makundi mbalimbali tukianza na tuzo ya mwanamke
bora mjasiriamali,wanawake bora wa kikundi wajasiamali pamoja na binti
mjasiriamali na kwa wanaume Kuna tuzo za kiongozi bora , mwanafunzi bora
mjasiriamali,pamoja na kiongozi bora"alisema Phide
Kwa
upande wake afisa utamaduni wa jiji la Arusha Elizabeth Ncheye
alipongeza kampuni hii ya Phide Intertaiment kwa kuandaa tuzo hizi
ambapo alizitaka kampuni zingine za sana ziendelee kuiga mfano huu wa
kuandaa tuzo mbalimbali kwani zinasaidia kutoa hamasa kwa jamii yetu na
kuwatia moyo wanajamii ambao wanajihisisha na shughuli nzima za
ujasiriamali ambapo alifafanua wakizungumzia ujasiriamali ndani yake
kuna ubunifu ndani yake kinapatikana kitu kinaitwa sanaa na ndio maana
baraza la sanaa linasimamia zoezi la tuzo
Aliwataka wanawake wengi ,wanafunzi na wanaume waweze kushiriki kwa wingi katika Tuzo hizi kwani zinasaidia Sana kuwatangaza na kukuza biashara zao zaidi.
Kwa upande mmoja wapo wawashindi wa Tuzo za wanawake ambaye pia ni mmiliki wa maduka ya nguo yajulikanayo kwa jina la new look braido , Elizabeth Mayani (mama shombee)alisema tuzo hizi zimeweza kumsaidia kukuza biashara yake kwani tangu ameweza kupata tuzo hii amepata kazi nyingi ikiwepo ya kumvalisha mtoto wa Mchungaji mkubwa duniani ajulikanae kwa jina TB Joshua ,ambapo alimvalisha mtoto wake wa kike ajulikanae kwa jina la Serah Katika harusi yake uliofanyika mkoani hapa.
Aliwataka wanaume na wanawake kushiriki tuzo hizi kwani zinasaidia kukuza biashara zao kwa haraka na zinawafanya wajulikane zaidi.
Tuzo hizo za wanawake zinafanyika kila mwezi tatu ya kila mwaka na kwa upande wa Tuzo za wanaume zitafanyika kila mwezi July 20 ya kila mwaka .





No comments :
Post a Comment