Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na vyombo vya habari jana Jijini Dar es salaam kuwa mashine za kupimia Virusi vya Korona kwa Watalii kwa sasa zimepelekwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti pamoja na Arusha ikiwa ni Juhudi za makusudi zilizochukuliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kukuza sekta ya utalii kwa kuondoa adha kwa Watalii wanaotembelea Vivutio vya Utalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Allan Kijazi mara baada ya kuwasili Jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuzungumza na Vyombo vya habari jinsi inavyochukua hatua katika kupambana na Ugonjwa virusi vya Corona ambao umeathiri sekta ya utalii nchini kwa zaidi y asilimia 50 ambao Wizara katika kukabiliana nao imepeleka mashine mbili kwa ajili ya kuwapimia Watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti pamoja na Arusha
No comments :
Post a Comment