Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MWANAMAMA
Marium Mtumbuka (29) mkazi wa Jijini Ilala Mkoa wa Dar es Salaam na
mwenzake Hamis Awadhi (44), wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu mbele ya mahakimu wawili tofauti wakikabaliwa na tuhuma za
kusafirisha zaidi ya kilogramu 13.15 za dawa za kulevya aina ya Heroin.
Katika
hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali
Faraja Ngukah mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Yusto Lubiroga imedai
kuwa, Aprili 2, 2021 huko uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, uliopo
Jijini Ilala Mkoa wa Dar es Salaam mshtakiwa Marium alikutwa
akisafirisha Kg 6.65 za dawa za kulevya aina ya Heroin.
Aidha
imedaiwa na wakili wa serikali, Ester Martin mbele ya Hakimu Mkazi
Mwandamizi Kassian Matembele kuwa, siku na mahali hapo mshtakiwa Awadhi
alikutwa akisafirisha kg 6.75 za dawa za kulevya aina ya Cocaine.
Hata
hivyo washtakiwa wote kwa nyakati tofauti hawakuruhusiwa kujibu kitu
chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina
mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida
kusikilizwa mahakama Kuu kitengo cha mafisadi.
Kwa
mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika hizo bado haujakamilika
na kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 27.2021 washtakiwa wamerudishwa
rumande.

No comments :
Post a Comment