Thursday, April 15, 2021

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AJUMUIKA NA WAFANYAKAZI WA OFISI YAKE KATIKA SALA YA ADHUHURI NA KUZUNGUNZA NA UONGOZI WA CHUO KIKUU HURIA TANZANIA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Ust Idrissa Matulubu, baada ya kumaliza kwa Sala ya Adhuhuri  ambapo alijumuika na Wafanyakazi wa Ofisi yake katika Msikiti ulioko eneo la Ikulu Jijini  Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Prof.Elifas Tozo Bisanda alipofika Ikulu Jijini Zanzibar na Ujumbe wa Uongozi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (haupo pichani) mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wahadhari wa Chuo Kikuu Huria Tanzania ukiongozwa na Makamo Mkuu wa Chuo Prof.Elifas Tozo Bisanda, walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania ukiongozwa na Makamo Mkuu wa Chuo Prof.Elifas Tozo Bisanda (kulia kwa Rais) na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu.(Picha na Ikulu)

 

No comments :

Post a Comment