Thursday, April 1, 2021

NMB yashiriki kukamilisha ndoto za wanafunzi Kanda ya Kaskazini


 

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Same, Mkoa wa Kilimanjaro,Juma Mpimbi akikagua meza na viti vilivyotolewa na benki hiyo katika Shule ya Sekondari Kwakoko wakati wa ziara ya kukagua matumizi ya vifaa hivyo hivi karibuni.

Wanafunzi wa kidato cha Nne Shule ya Sekondari Kwakoko wilaya ya Same ,Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa wamekalia meza na viti zilizotolewa msaada na Benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya benki hiyo kurejesha faida kwa jamii.

Wanafunzi wa kidato cha Nne Shule ya Sekondari Kwakoko Wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa wamekalia meza na viti zilizotolewa msaada na Benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya benki hiyo kurejesha faida kwa jamii.


=======  =======  ========

Wanafunzi katika Shule za Sekondari imani yao kubwa katika kufaulu na kuhudhuria madarasa kwa

furaha ni namna ambavyo Mwalimu anatoa ujuzi wake kwa kujiamini, mpangilio wa darasa lakini zaidi ni mazingira na vifaa vya kufundishia.

Kwa kuliona hilo, Benki ya NMB kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii wametenga kiasi cha asilimia moja ya faida ili kusaidia mambo mbalimbali ikiwemo elimu, afya na majanga mengine ya asili mara yatokeapo.

Miongoni mwa Shule walizosaidia ni Shule ya Sekondari Kibacha na Shule ya Sekondari Kwakoko zilizopo Mkoani Kilimanjaro, Wilaya ya Same, ambapo wanafunzi wanasema fadhila pekee wanayoweza kuwalipa NMB pamoja na wazazi wao ni kusoma kwa bidii.

NMB imesaidia viti 50 na meza zake katika Shule ya Sekondari Kwakoko ambapo pia wamesaidia viti 50 na meza zake katika Shule ya Sekondari Kibacha pamoja na vifaa vya maabara za Sayansi za kujifunzia wanafunzi.

Wakizungumza katika nyakati tofauti wanafunzi wa Shule hizo, walisema wanajiona wana bahati kuwa sehemu ya utaratibu huo wa NMB kwa kuwa awali walisoma katika mazingira magumu lakini hawakuwa na namna ya kufanya.

Nasra Selemani mwanafunzi wa Kidato cha Nne A Shule ya Sekondari Kibacha, anasema: “Tulikuwa wanyonge sana wakati tukikaa chini, hasa sisi wasichana kwa kuwa tulichafuka. Hatukuwa na utulivu wakati wa masomo kwa sababu wakati mwingine tulikaa wawili kiti kimoja. Lakini tangu tupokee msaada huu wa viti na meza kutoka NMB hata ufaulu umeongezeka na wanafunzi hawategei masomo.”

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibacha, Omary Magongo alisema   wamefaidika kwa kiasi kikubwa na NMB, wana wanafunzi hadi 800 ambapo walipeleka kuwa na uhaba wa madawati, lakini NMB iliwasaidia kutatua.

Naye mwakiliki wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Kwakoko, Mwalimu Naiman Kavumo alisema walikuwa na uhaba wa viti kati ya 65 hadi 100, lakini viti na meza 50 walizopokea kutoka NMB vimewapa faraja na hata wanafunzi wameonyesha nia ya dhati ya kufanya vizuri.

Akielezea namna msaada huo unavyopatikana Afisa Uwajibikaji kwa Jamii wa NMB, Aloyce Kikois, alisema wengi wanadhani msaada huo unapatikana kwa kuandika barua ndefu au inayohitaji utaalamu mkubwa, lakini yeyote anaweza kuandika na kupeleka maombi hayo kwa Meneja wa Tawi la NMB lililopo karibu naye, lakini hakikisha unaainisha mahitaji,  jina la shule, wilaya na mkoa ilipo shule.

No comments :

Post a Comment