MTEJA
wa Kampuni ya Vodacom Francis Mosha amefungua kesi ya madai dhidi ya
Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania akidai fidia ya shilingi Milioni 26
kwa kumkata kiasi cha shilingi 2936 kwenye akaunti yake ya M-Pesa.
Madai
hayo namba 57 ya mwaka 2021 yapo katika Mahakama ya wilaya ya Kinondoni
mbele ya hakimu Mkazi Happy Kikoga ambapo leo Aprili 15, 2021 yaliitwa
mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.
Katika
madai yake, Mosha kupitia wakili wake Michael Merere anadai
kwambaJanuari 8, 2020 bila sababu za msingi kupitia akaunti yake ya
M-pesa kiasi cha sh. 20,000 kilikatwa na kwamba tatizo hilo lilijirudia
Januari 9, 2021 ambapo kiasi cha shilingi 9136 kilikatwa kutoka katika
akaunti yake ya M-Pesa.
Amedai
baada ya Matukio hayo mawili mlalamikaji aliwasiliana na muhudumu wa
Vodacom ambaye alimweleza tatizo hilo litafanyiwa kazi, lakini miezi
mitatu ilipita na hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa na Vodacom.
Kufuatia
hali hiyo ya uzembe wa Vodacom au kushindwa kutilia maanani madai yake
mdai, aliamua kuajiri Mwanasheria ambaye alipeleka madai kwa
walalamikiwa, pamoja na kupolekewa barua hiyo, majibu ya Vodacom
yalikuwa si ya kurudhisha kwa kuzingatia kuwa pesa za Mdai
hazikurudishwa kwa takribani miezi minne, kitendo hicho kilimsababishia
hasara hiyo.
Kufuatia hasara hiyo Mosha anaiomba Mahakama waiamuru Vodacom imlipe fedha hizo kiasi cha shilingi 26496320.
Hata
hivyo katika majibu ya Vodacom Tanzania kupitia wakili wake Elizabeth
Chacha wamekanusha madai hayo na kuwasilisha pingamizi la awali
wakiiomba Mahakama itupilie mbali ombi hilo kwa sababu Mahakama hiyo
haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.
Pia
wamedai kuwa madai hayo si ya kweli na kwamba hakuna hasara yeyote
ambayo Mdai ameipata kwa sababu hela hizo zilikatwa kimakosa na
zilisharudishwa.
Kesi
hiyo imeahirishwa hadi Aprili 21, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa ili
kuipangia tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa pingamizi hilo kabla ya kesi
ya msingi.
No comments :
Post a Comment