****************************************
NA SULEIMAN MSUYA
MSHINDI wa Kwanza wa
Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’an yanayoandaliwa na Taasisi ya
Al-Hikma anatarajiwa kupewa zawadi ya nyumba nyenye thamani ya shilingi
milioni 40.
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi wa Taasisi ya Al-Hikma, Sheikh Nurdin Kishk wakati
akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Temeke jijini Dar es Salaam.
Sheikh Kishk amesema zawadi hiyo imetolewa na Benki ya Mwananchi Zanzibar (PBZ) iwapo mshindi wa kwanza atakuwa Mtanzania.
Amesema iwapo mshindi
wa kwanza hatakuwa Mtanzania Taasisi ya Al-Hikma itatoa shilingi
milioni 20 na zawadi zitakuwa kwa mshindi wa kwanza hadi watano.
Kishk amesema mashindao ya mwaka huu yatashirikisha washiriki 23 kutoka nchi 21 za Bara la Afrika.
“Mashindano ya mwaka
huu yatafanyika April 25 katika Uwanja wa Banjamin Mkapa ambapo mshindi
wa kwanza akiwa Mtanzania PBZ itatoa nyumba yenye thamani ya shilingi
milioni 40.
Ila sisi kama waandaji tumetenga shilingi milioni 20 kwa mshindi wa kwanza iwapo hatakuwa Mtanzania,” amesema.
Mkurugenzi huyo
ametaja baadhi ya nchi ambazo zitakuwa na washiriki ni pamoja na
Tanzania, Zanzibar, Kenya, Uganda, DRC Congo, Senegali, Afrika Kusini na
Burundi.
Aidha amesema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar, Dk.A
Hussein Mwinyi na Mgeni Maalum atakuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Sheikh Kishk
amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye mashindao hayo ambayo
yamekuwa na mafanikio makubwa kwa miaka 20 iliyopita.
Kwa upande wake Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe ameipongeza Taasisi ya Al-Hikma kwa
kuandaa mashindano hayo ambayo yanachangia kujenga jamii yenye kumcha
Mungu na nidhamu.
Gondwe amesema wilaya itatoa ushirikiano wa hali ya juu kuhakikisha mashindani hayo yanafanyika kwa usalama na mafanikio.
“Nawapongeza Al-Hikma
kwa kuandaa mashindao haya kwani yamekuwa na matokeo chanya tangu
yaanze. Naomba washiriki wa Tanzania mjitahidi kubakiza ushindi hapa,”
amesema.
Aidha, Mkuu wa Wilaya
Gondwe amewataka wafanyabiashara kuacha tabia ya kuongeza bei ya bidhaa
katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
No comments :
Post a Comment