Wanahabari
tofauti kutoka Tanzania wakibadika karatasi ambazo zinalenga kuonesha
ni vitu gani wanapaswa kufanya wanaume na vitu gani ambavyo vinapaswa
kufanya wanawake na ni vipi wanaweza kufanya wote kwa pamoja.
Mwandishi
wa habari kutoka gazeti la Daily news kwa upande wa Zanzibar Issa
Yussuf akichangia miongoni mwa mada zilizowasilishwa katika mafunzo
hayo.
Mwakilishi
wa shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa.UNESCO
Nacy Kaizilege akitoa neon kwa niaba ya shirika hilo.
Mkurugenzi
wa TAMWA Rose Reuben akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa
habari 30 Tanzania yenye lengo la kuwawezesha wanahabari hao kuandika
habari za kijinsia pamoja na umuhimu wa uongozi kwa wanawake.
Baadhi
ya waandishi wa habari kutoka vyombo tofauto wakijianda kubadika
karasai ambazo zinalenga kuonesha ni mambo gani anayostahiki kufanya
mwaname na mwanamke.
Na Muhammed Khamis, TAMWA
Aliyasema
hayo katika ukumbi wa White Sand hote Mbezi Jijini Dar Es Salam katika
mafunzo maalumu ya siku tatu ya waandishi wa habari 30 kutoka vyombo
tofauti Tanzania yaliolenga kuwajenga uwezo waandishi hao kuhusu maswala
ya kijinsia na umuhimu wa uongozi kwa wanawake.
Alisema
wanawake katika jamii bado wanaonekana si watu wenye kustahiki kuwa
viongozi na ndio maana uwepo wa Rais Samia madarakati hadi leo hii kuna
watu wanaendelea na mshangao.
Kufuatia
dhana hiyo Mkurugenzi huyo alisema waandishi wa habari ndio wenye
wajibu wa kubadili mitazamo hio kwa jamii ili waweze kuamini kuwa
mwanamke ni kama sehemu nyengine ya wanaopaswa kuwa viongozi.
Alisema
kwa kuwa wanahabari wana sauti kubwa kuliko watu wengine ama taasisi
basi wanapaswa kutumia vyema fursa walionayo kuibadili jamii ya
kitanzania kutoka kwenye mawazo yasiopaswa kuwepo hadi sasa.
‘’Tunahitaji
kuona mifumo ya usawa kwenye jamii zetu ili wanawake wasiedelee
kuonekana kuwa watu dhaifu na wasiofaa kushika nafasi mbali mbali za
uongozi.’’Aliongezea.
Kwa
upande wake mwakilishi wa Shirika la umoja wa kimataifa linalojihusisha
na maswala ya wanawake UNWOME Hodan Addov alisema wataendelea
kushirikia na TAMWA katika pande zote mbili kwa lengo kwa lengo la
kuleta usawa katika jamii.
Alieleza
kuwa anaamini uwepo wa usana ni dhana inayostahiki kuwepo kwa lengo la
kujenga Tanzania imara kwa watu waote bila upande mmoja wa jinsia
kuonekana kuwa na nguvu zaidi na mwengine ni dhaifu.
Nae
mwakilishi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa
Mataifa.UNESCO Nacy Kaizilege alisema wanahabari wanawajibu kupasa
sauti zaidi za wanawake kupitia taarifa zao za kila siku huku wakijua
kuwa wanawake ni watu wanaohitaji kupaziwa sauti zao zaidi.
Sambamba
na hilo aliwataka pia wanahabari hao kutoacha kupaza sauti zao kuhusu
maswala ya udhalilishaji katika Nyanja mbali mbali zikiwemo za kisiasa
ambapo hadi sasa kumekuwepo na taarifa mbali mbali za udhalilishaji kwa
wanawake kupitia siasa.
No comments :
Post a Comment