Balozi
wa Denmark nchini Tanzania, Mette Norgaard Dissing-Spandet (kushoto) na
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu
Ng’wanakilala (kulia) wakisaini mkataba wa ruzuku ya nyongeza kiasi cha
shilingi za kitanzania 5.6 bilioni (USD 2.4 million) zilizotolewa na
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Denmark (DANIDA) kwa ajili ya
kutekeleza mradi wa upatikanaji wa haki nchini kwa kipindi cha mwaka
mmoja kati ya Januari na Desemba 2021 unaotekelezwa na LSF.
Balozi
wa Denmark nchini Tanzania, Mette Norgaard Dissing-Spandet (kushoto) na
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu
Ng’wanakilala (kulia) wakibadilishana nyaraka za makubaliano baada ya
tukio la kutiliana saini mkataba wa ruzuku ya nyongeza kiasi cha
shilingi za kitanzania 5.6 bilioni (USD 2.4 million) zilizotolewa na
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Denmark (DANIDA) kwa ajili ya
kutekeleza mradi wa upatikanaji wa haki nchini kwa kipindi cha mwaka
mmoja kati ya Januari na Desemba 2021, unaotekelezwa na LSF.
Balozi
wa Denmark nchini Tanzania, Mette Norgaard Dissing-Spandet (kushoto) na
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu
Ng’wanakilala (kulia) wakifurahia pamoja baada ya tukio la kutiliana
Saini kwa mkataba wa ruzuku ya nyongeza kiasi cha shilingi za kitanzania
5.6 bilioni (USD 2.4 million) zilizotolewa na Shirika la Maendeleo la
Kimataifa la Denmark (DANIDA) kwa ajili ya kutekeleza mradi wa
upatikanaji wa haki nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja kati ya Januari
na Desemba 2021 unaotekelezwa na LSF.

Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu
Ng’wanakilala akisaini mkataba wa ruzuku ya nyongeza kiasi cha shilingi
za kitanzania 5.6 bilioni (USD 2.4 million) zilizotolewa na Shirika la
Maendeleo la Kimataifa la Denmark (DANIDA) kwa ajili ya LSF kutekeleza
mradi wa upatikanaji wa haki nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja kati ya
Januari na Desemba 2021.

Balozi
wa Denmark nchini Tanzania, Mette Norgaard Dissing-Spandet akitia saini
mkataba wa ruzuku ya nyongeza kiasi cha shilingi za kitanzania 5.6
bilioni (USD 2.4 million) zilizotolewa na Shirika la Maendeleo la
Kimataifa la Denmark (DANIDA) kwa ajili ya kutekeleza mradi wa
upatikanaji wa haki nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja kati ya Januari
na Desemba 2021 unaotekelezwa na LSF.
Kiasi
cha Shilingi bilioni 5.6 (USD 2.4) Kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa
upatikanaji wa haki nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja kati ya januari
hadi mwishoni mwa disemba mwaka huu.
Ruzuku
hiyo iliyopokelewa inalenga kuboresha Mazingira ya Uwekezaji wa
kisheria nchini kwa kuzijengea uwezo Taasisi zinazotoa huduma ya msaada
wa kisheria pamoja na huduma za wasaidizi wa kisheria kwa makundi
mbalimbali katika jamii hususani wanawake na watoto.
Akizungumza
wakati wa hafla ya utiaji saini,Balozi wa Denmark nchini Mette
Norgaard amesema kuwa Shirika la Maendeleo Kutoka Denmark (DANIDA)
imeamua kuwaongezea ruzuku Shirika linalotoa msaada wa kisheria nchini
(LSF) kama sehemu ya uwajibikaji katika kuhakikisha suala la upatikanaji
haki nchini linazingatiwa.
"Shirika
linalotoa msaada wa kisheria(LSF) limekua mdau wetu mkubwa takribani
miaka 10 na tumeamua kuongeza ruzuku hiyo ili kusaidia zaidi utekelezaji
wa mradi wa (LSF) unaotekelezwa kwa ajili ya kusaidia wakina Mama na
watoto ambao ndio wahanga wakubwa wa maswala ya haki zao." Amesema
Mette.
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika linalotoa Msaada wa kisheria
nchini (LSF) Lulu Ng'wanakilala amesema kuwa ruzuku iliyotolewa na
wadau wake itasaidia kikamilifu katika kuendelea kutekeleza Mradi wa
upatikanaji wa haki nchini unaotekelezwa nchi nzima kwa upande ea
Tanzania bara na visiwani Zanzibar.
Ng'wanakilala
ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (LSF) imekuwa
imishirikiana na wadau wake mbalimbali ikiwemo Shirika la Maendeleo
Kutoka Denmark (DANIDA) ambapo imeweza kusaidia kuboresha sekta ya
msaada wa kisheria nchini kupitia uwezeshaji wa kisheria zaidi ya 4000
nchi nzima
Pia
aliongeza kuwa Wanaamini ruzuku hii itawasaidia katika kuboresha Mifumo
ya utoaji haki iliyo rasmi na isiyo rasmi ili kuwezesha upatikanaji
haki kwa wakati.



No comments :
Post a Comment