Na Woinde Shizza, Michuzi Tv -ARUSHA
MLALAMIKAJI
katika kesi ya wizi wa sh,milioni 300 namba 87 ya mwaka 2020, Emmanuel
Wadoo maarufu kwa jina la Sunda ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa
Madini na mmiliki wa hotel ya kitalii ya Mount Meru jijini Arusha
,amejikuta akiangua kilio mahakamani katika kesi hiyo ambayo anamtuhumu
mfanyakazi wake wa ndani (houseboy) kumwibia mamilioni ya fedha hizo.
Wadoo
ambaye ni shahidi namba moja katika Shauri hilo,alilazimika kuangua
kilio huku akitokwa na jasho jingi na kuagiza maji ya kunywa mara kwa
mara mahakamani hapo wakati akihojiwa na wakili wa upande wa utetezi,
Edmund Ngemela baada ya kubanwa kuhusu madai yake ya kwamba nyumba yake
haina uzio, haijafungwa cctv camera na hana mlinzi wala wafanyakazi wa
ndani na alikuwa akiishi yeye na mke wake tu wakati tukio hilo likitokea
Hata
hivyo shahidi wa pili , Jeremiah Mchome,alitofautiana na mlalamikaji
huyo baada ya kuieleza mahakama kwamba nyumba ya mfanyabiashara huyo
imefungwa camera na ana wafanyakazi watatu wa kike, uzio na mlinzi na
kwamba hakumwona mtuhumiwa akiiba kiasi hicho cha fedha bali aliambiwa
na mlalamikaji.
Shauri
hilo linalosikilizwa na hakimu Pamela Meela wa makahama ya hakimu
Mkazi wilaya ya Arumeru ,Wadoo anamlalamikia Joel Keya ambaye alikuwa
Mtunza bustani nyumbani kwake eneo la PPF Njiro, jijini Arusha .
Wado
aliiambia mahakama hiyo jana kwamba Joel Keya akiwa mfanyakazi wake
kati ya April na June mwaka 2018 na alimwibia Madini ya Tanzanite yenye
thamani ya sh,milioni 60, dola 7000 za kimarekani, fedha taslimu sh.
milioni 200, na simu aina ya iPhone vyote vikiwa na thamani ya
sh,milioni 300.
Wakili
Ngemela alimhoji mlalamikaji kwanini hakutoa taarifa kituo Cha polisi
tangu mwaka 2018 wizi ulipotokea hadi mwaka 2020 alipoamua kutoa taarifa
polisi ,Wado alieleza kwamba alikuwa akifanya uchunguzi na baadaye
alielezwa na mke wake kwamba Joel ndiye amekuwa akimwibia kwani siku
moja alirudi nyumbani na alipoingia ndani alikuta kabati la fedha
limevunjwa na alipotoka nje alimwona Joel akiondoka na pikipiki. .
Naye
shahidi wa tatu, Jackson Marunda(39) Mkazi wa Olorien ambaye ni mwosha
magari kwa mlalamikaji alisema mnamo desemba 19 ,2019 akifanya kazi ya
kuosha gari ya mlalamikaji alimwona Joel Keya akitoka ndani kupitia
dirisha la choo Katika nyumba ya mlalamikaji.
Huku
akiongozwa na wakili wa serikali Grace Mesikenya alisema kuwa taarifa
za wizi alizisikia kituo cha polisi baada ya kuitwa na kumkuta mtuhumiwa
akiwa chini ya ulinzi .
Shahidi
alieleza kwamba desemba 27 mwaka 2019 alifika nyumbani kwa mlalamikaji
kwa ajili ya shughuli za kuosha magari lakini mlinzi wa eneo hilo
alimwambia asiingie ndani kwani Kuna wizi umetokea.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi April 20, mwaka huu ambapo itaendelea kwa upande wa mashtaka kutoa ushahidi.
No comments :
Post a Comment