Friday, April 9, 2021

KATIBU MKUU NZUNDA: WATUMISHI TOENI USHAURI WENYE WELEDI KWA VIONGOZI WENU


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda akizungumza wakati wa kikao cha kumuaga aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko kilichofanyika katika ofisi hizo Jijini Dodoma tarehe 9 Aprili, 2021.

Aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza jambo wakati kikao cha kumuaga rasmi katika ofisi hiyo, kilichofanyika tarehe 9 Aprili, 2021 katika Ofisi hiyo Dodoma.Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa ofisi hiyo (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda.

Aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza jambo wakati kikao cha kumuaga rasmi katika ofisi hiyo, kilichofanyika tarehe 9 Aprili, 2021 katika Ofisi hiyo Dodoma.

Aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akipokea zawadi ya vitenge kutoka kwa Wakurugenzi Wasaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa ofisi hiyo, Bi. Mazoea Mwera (mwenye ushungi) na wa kwanza kulia ni Vedastina Justinian wakati wa kikao hicho.

Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Bajeti wa ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Eleuter Kiwelle akizungumza kwa niaba ya watumishi wa ofisi hiyo wakati wa kikao cha kumuaga aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi. Dorothy Mwaluko.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko (mwenye miwani) wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ofisi hiyo mara baada ya kumuaga rasmi katika ofisi hiyo, Aprili 9, 2021.

 (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

………………………………………………………………………………….

MWANDISHI WETU

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye

Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda amewaasa watumishi wa ofisi yake kuendelea kutoa ushauri wenye weledi na kuzingatia taaluma katika kusaidia masuala ya Uratibu wa Shughuli za Serikali katika ofisi yake.

Kauli hiyo ameitoa mapema hii leo Aprili 9, 2021 wakati wa kikao cha kumuaga aliyekuwa katibu Mkuu wa ofisi hiyo (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko katika ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo Mtaa wa Reli Dodoma.

Aliwaeleza kuwa viongozi wanatambua michango na ushauri wanaotoa kila wakati na kuhimiza waendelee kufanya hivyo bila kusita ili kuendeleza kasi ya utendaji katika ofisi yake.

“Ikumbukwe kuwa mshauri kazi yake si, kushauri mambo mazuri tu ambayo viongozi wangependa kuyasikia bali kutoa ushauri wenye weledi na kuzingatia taaluma na ifanyike hivyo hata kama wakuu hao wasingependa kusikia ukweli huo”

Kwa upande wake aliyekuwa katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi. Dorothy mwaluko akizungumza na watumishi hao amewaasa watendaji wa ofisi hiyo kuendelea kuchapa kazi kwa ufanisi na kuendana na kazi ya Serikali yetu.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Bajeti wa ofisi hiyo Bw. Eleuter Kiwelle kwa niaba ya watumishi wa ofisi hiyo aliahidi kuenzi kwa vitendo yale mazuri waliojifunza kwa uongozi wa aliyekuwa katibu mkuu Bi. Mwaluku na kuahidi kuendelea kumuombea heri katika utuimishi wake wa umma.

“Kwa niaba ya watumishi wote, tunakushukuru kwa zawadi ya uwepo wako katika ofisi hii, na tunaahidi kuendeleza mazuri yote na kudumu katika nidhamu na weledi kiutendaji ili kuendeleza kasi ya maendeleo,”alisema Kiwelle.

“Tumejifunza mambo mengi kwako na kuonja upendo wako kwetu, hivyo tunaahidi kuendelea kuyaenzi katika utumishi wetu umma,”alisisitiza

 

No comments :

Post a Comment