Mkurugenzi
wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Wizara ya Mawasiliano Zanzibar, Dkt.Mzee
Suleiman Mndewa (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya Pasua Anga Ki Zantel 4G uliofanyika kupitia televisheni ya
ZBC.Kulia ni Mkuu wa Zantel Zanzibar Mohammed Khamis Mussa pamoja na
Zuena Ali (mjasiriamali). Kampeni hiyo imelenga kuelimisha umma juu ya
umuhimu wa matumizi ya mtandao wa 4G katika kujiletea maendeleo.
Mkuu
wa Zantel-Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa akizungumza wakati wa
uzinduzi wa kampeni ya Zantel ijulikanayo kama ‘Pasua Anga Ki Zantel
4G’. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uchukuzi-Wizara ya
Mawasiliano Zanzibar, Dkt.Mzee Suleiman Mndewa na Zuena Ali mjasiriamali
mdogo. Kampeni hiyo imelenga kuelimisha umma juu ya umuhimu wa matumizi
ya mtandao wa 4G katika kujiletea maendeleo.
Mkuu
wa kitengo cha biashara wa Zantel, Aneth Muga akicheza mchezo wa
Foosball pamoja na Mohammed Waziri mmoja wa wananchi waliofika katika
uzinduzi wa kampeni ya ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’ uliofanyika katika
viwanja vya Kisonge Unguja.Kampeni hiyo imelenga kuwaelimisha wateja juu
ya umuhimu wa mtandaowa 4G katika kujiletea maendeleo ya kijamii na
kiuchumi.
==== ====== ======= ====
Kampuni
ya simu ya Zantel leo Machi 16, 2021 imezindua kampeni yake mpya
ijulikanayo kama ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’ inayolenga kuwaelimisha
wateja juu ya uhumimu wa mtandao wa 4G katika kujiletea maendeleo.
Uzinduzi
huo umefanyika leo katika viwanja vya Kisonge mjini Unguja ambapo
wananchi wameweza kushiriki na kujionea ni namna gani wanaweza kutumia
mtandao wa 4G kwa manufaa ya kijamii na kiuchumi.
Kabla
ya uzinduzi huo, Kampuni ya Zantel iliendesha mjadala ulijadili juu ya
umuhimu wa mtandao wa 4G ambao uliruka kupitia televisheni ya
ZBC.Mdahalo huo ulihusisha wadau mbalimbali kutoka Serikalini pamoja na
wajasiriamali.
Akizungumza
wakati wa mjadala huo, Mkuu wa Zantel Zanzibar Mohammed Khamis Mussa
alisema “Nia yetu ni kunaendelea kuboresha mtandao wetu ili mawasiliano
yapatikane Zanzibar yote kwa kasi ya 4G kumuwezesha mtumiaji kuweza
kufanya mawasiliano bora na ya haraka. Na sasa tunazindua kampeni ya
PASUA ANGA ki ZANTEL 4G mahsusi ili kutoa elimu kwa umma juu ya manufaa
mbalimbali ya mtandao ulioboreshwa wa Zantel 4G.”
Katika
uzinduzi uliofanyika viwanja vya kisonge, ulihusisha shughuli
mbalimbali ikiwamo michezo ya foosball, tebal tennis, pool table huku
washindi wakiibuka na vifurushi vya intaneti ya 4G vya wiki pamoja na
zawadi mbalimbali.
No comments :
Post a Comment