Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Imelda Salum akimpatia maelezo Waziri wa Mawasiliano Tehana Habari Faustine Ndungulile namna kifaa Cha kukagua mwingiliano wa masafa kinavyofanya kazi.
Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari aliendelea kupokea maelezo namna kifaa hicho kinafanya kazi na kuhakikisha hakuna mwingiliano wa masafa Kati ya mtoaji wa huduma na mwingine.
Wa kwanza kulia ni Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Faustine Ndungulile akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Posta mkoa wa Arusha Athuman Msilikale akiye kulia kwake ni Posta masta mkuu Hassan Mwang'ombe
Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Faustine Ndungulile akimsikiliza kwa makini Meneja wa Posta mkoa wa Arusha Athuman Msilikale,wa kwanza. Kushoto Ni Posta masta mkuu Tanzania Hassan Mwang'ombe
Wa kwanza kushoto Ni Posta masta mkuu Tanzania Hassan Mwang'ombe akifuatiwa na Meneja wa Posta mkoa wa Arusha Athuman Msilikale (aliye vaa shati la blue)akitoa taarifa kwa Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Faustine Ndungulile alipotembelea kuona utendaji kikazi
Baadhi ya wafanyakazi wa posta Mkoani Arusha
Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Faustine Ndungulile akipokea maelezo kutoka kwa Posta masta mkuu Kama inavyoonekana katika Picha.
Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Imelda Salum akiwasilisha ripoti fupi ya utendaji kwa Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Faustine Ndungulile alipotembelea ofisi za Kanda Jijini Arusha leo.
Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Faustine Ndungulile akizungumza na wafanyakazi wa posta hawapo pichani aliye kulia kwake Ni Posta masta mkuu na Meneja wa Posta mkoa wa Arusha
Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Faustine Ndungulile akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa afanyakazi wa TTCL alipotembelea ofisi hiyo Kuona maendeleo yao kiutendaji
Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Faustine Ndungulile akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa posta Mkoani Arusha
Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Faustine Ndungulile akiwa katika Picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TTCL alipotembelea Kuona maendeleo yao kiutendaji
Na.Vero Ignatus,Arusha
WIZARA Mawasiliano na Teknoloji ya Habari imeitaka Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA )Kupunguza muda wa kusajili leseni za Maudhui ya mitandaoni ili inapofika mwazoni mwa mwezi Mei vijana na wananchi wawezekujikwamua kiuchumi kwa kuitumia mitandao hiyo
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nchini Faustine Ndungulile wakati akiwa katika kikazi Mkoani Arusha iliyoanza leo ambapo alitoa muda wa mwezi mmoja kuhakikisha Sheria zote zimepitiwa na muda wa usajili wa mitandao hiyo umefunguliwa
Ndungulile amesema kuwa ni vyema Mamlaka hiyo ikajikita zaidi kutoa Elimu kwa jamii kwani na ni kosa kisheria kutumia mtandao wa kijamii bila kusajiliwa
Aidha ameipongeza TCRA Kanda ya Kaskazini kwa kutoa Elimu kwa mafundi simu na kusema kuwa Elimu hiyo itawasidia mafundi hao na kutambulika kisheria ambapo aliraka Kanda zingine kuiga mfano huo.
"Niwaonye mafundi simu wote wale maabao wanafuta IMEI namba za simu ambazo zimeibiwa na kuweka IMEI namba moya waache maara moja kwani Wizara yangu Ina mashine ambazo hata ukifuta simu inatambua na tukiwabaini tutawwchukulia hatua Kali za kisheria"alisema
Ndungulile amewataka wananchi kufahamu kuwa ifikapo Juni 30 laini zote za simu ambazo hazijasajiliwa kwa Alama za vidole zitgungwa kwani Serikali ilishatoa muda mrefu kwa wananchi kusajili kwa alama za vidole
Akiongea katika ofisi ya posta waziri aliwataka wafanyakazi kuongeza ubunifu zaidi pamoja na Kuongeza ufanisi Katika utendaji wao wa kazi ,huku akiwataka watumishi wa posta ambao hawajui kompyuta kwenda kujifunza, kwani iwapo huduma za namba ya simu kuwa sanduku lako la posta (virtual box )zikianza hawatakuwa na kazi Kama hawana ujuzi
Alitaka wizara yake kuharakisha mabadiliko ya sheria ,ikiwemo mabadiliko ya sera ya posta ambapo pia aliwataka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kusimamia sheria ya usafirishaji ,huku akiwasisitiza majukumu ya posta yalindwe Ila kwenye kazi wakafanye kazi vyema bila kuingiliana
"TCRA mnafanya usajili wa vyombo vinavyofanya biashara ya usafirisha hivyo msitoe leseni tu na kuwaacha bali mtoe leseni na kuwafatilia hao ambao mnawapa leseni Kama wanafanya kazi kwa kufuata sheria"alisema Ndugulile
Kwa upande wake meneja wa Kanda ya kaskazini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Muhandisi Emelda salumu alisema kuwa Kanda ya kaskazini kwa mwaka wa fedha 2020 /2021 wameweza kutekeleza majukumu yao kwa kushughulikia maombi ya leseni ambapo walipokea maombi 54 ambapo 51 yalishughulikiwa na 3 hayakufanikiwa kwasababu yalikuwa ni ya maaudhui mtandaoni na Mamlaka ilisitisha kwa muda
Aidha waliweza pia kufanya upimaji wa ubora wa matumizi ya Mawasiliano ya simu za mkononi,ufuatiliaji wa masafa na kuhakikisha yanatumika ipasavyo,ukaguzi wa watoa huduma za mawasiliano,watoa huduma kwanmaudhui ya kebo na mtandaoni na kufanya uelimishaji kwa wananchi watambue haki na wajibu wao
Alisema katika kuhakikisha uhalifu kupitia mitandao ya simu unapungua wameamua kutoa elimu kwa wananchi pamoja na mafundi simu ambapo mafunzo 332 wamepatiwa kwa upande wa Kanda ya kaskazini Arusha 123 Tanga 64 na Manyara 78 na Kilimanjaro 67 ambapo kwa Manyara bado wapi kwenye mafunzo
Alisema mafunzo haya yatawasaidia kuwa na ufanisi katika kazi zao pia wataona utofauti Kati yao waliopewa mafunzo pamoja na wale ambao hawakupewa mafunzo.
No comments :
Post a Comment