WATUMISHI WA WIZARA WAHIMIZWA KUFANYA KAZI KWA UWELEDI NA NIDHAMU.
Shemu nyingine ya Watumishi wa Wizara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo |
Shemu nyingine ya Watumishi wa Wizara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amewahimiza Watumishi wa Wizara kufanya kazi kwa kujituma, weledi na
nidhamu. Amesema haya alipokuwa akifungua mafunzo maalumu ya siku tano kwa Watumishi wa Wizara yanayoendelea jijini Dodoma.Katibu Mkuu amewakumbusha na
kusisitiza kuwa, Watumishi wa Wizara wakati wote wakiwa katika
utekelezaji wa majumu yao iwe ndani au nje ya mipaka ya nchi, wanapaswa
kuielewa na kuzingatia miongozo mbalimbali inayotumiwa na Wizara.
Ameitaja baadhi ya miongozo hiyo kuwa ni pamoja na Sera ya Mambo ya Nje,
Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Ilani ya CCM ya Mwaka 2020-2025,
Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati
anafungua Bunge la 12, Mpango Mkakati wa Wizara ambao huhuishwa kila
mwaka wa fedha, na sheria na kanuni zinazoongoza utumishi nje. Aliongeza
kuwa Mkataba wa Vienna (Vienna Convention) wa Mwaka 1961 na ule wa
mwaka 1963 unaohusu mahusiano ya kidiplomasia na mahusiano ya kikonseli
mtawalia pamoja na Kanuni za Utumishi Nje za Mwaka 2016 pia ni muhimu
zizingatiwe.
“Natambua ni ndoto ya kila Afisa
Mambo ya Nje (Foreign Service Officer) ni kwenda posting siku moja, kwa
mtakaobahatika kupata fursa ya kwenda kwenye Balozi zetu, mjue kwamba
mna deni kubwa kwa nchi yenu. Mnawiwa kutekeleza majukumu yenu kwa
kujituma, uzalendo, na kuhakikisha ulinzi na usalama wa maslahi ya nchi
yetu.” Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge.
Licha ya mafunzo hayo kulenga
kuwasaidia watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki kuelewa misingi bora ya maadili ndani ya Utumishi wa Umma,
Balozi Brigedia Jenerali Ibuge ameeleza mataumani yake kuwa mafunzo hayo
yatawasaidia watumishi kupata uelewa wa jumla kuhusu Maslahi ya Taifa,
Diplomasia ya Uchumi, Itifaki, Usalama wa kimtandao na utendaji wa kazi
katika mazingira ya kimataifa.
No comments :
Post a Comment