Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) akisalimiana na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) akiongea na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Balozi wa Vatican nchini Mhe.
Askofu Mkuu Marek Solczynski akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) wakati
walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar
es Salaam.
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika MAshariki, Mhe. William Tate Ole Nasha akiongea na Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika MAshariki, Mhe. William Tate Ole Nasha wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
****************************************
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Tanzania na Vatican zimeahidi kuendelea kuhimiza amani na utulivu katika masuala yenye
changamoto mbalimbali ili kuwezesha uwepo wa amani na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Baba Mtakatifu katika kuhimiza amani, utulivu na usalama duniani.Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) wakati alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski leo jijini Dar es Salaam.
Prof. kabudi amesema kuwa mazungumzo yake na Askofu Mkuu Solczynski yalijikita zaidi kuhusu umuhimu wa Tanzania na Vatican kushirikiana katika mikutano ya Umoja wa Mataifa kuhimiza amani, utulivu na mshikamano katika masuala mbalimbali yenye changamoto kwa binadamu.
“Tumeongelea umuhimu wa kulinda amani, utulivu na usalama duniani kote hasa katika maeneo yanayokumbwa na matatizo ya vita…….. katika hilo pia tuliongela suala la amani na usalama katika ukanda wa nchi za maziwa makuu, Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika tukijua kuwa kuna maeneo yanayohitaji amani ikiwemo eneo la kaskazini mwa Masumbiji, na mashariki ya Demokrasia ya Kongo,” Amesema Pro. Kabudi
Prof. Kabudi ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni na hata sasa dunia inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji mshikamano wa mataifa yote duniani ili kuweza kuyakabili hii ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu amani, utulivu, majanga, na magonjwa ya mlipuko kama vile Covid 19, na yale yanayohusu umasikini na hali yamaisha ya watu kubaguliwa na kuonewa.
“Mfano katika mapambano dhidi ya Uviko 19, Vatican na Baba Mtakatifu wanayo nafasi kubwa ya kutoa mchango wao katika eneo hilo katika kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya Covid 19 hayageuzwi kuwa katika masuala ya kibiashara na kisiasa na badala yake mapambano hayo yazingatie utu, undugu na imani, Ameongeza Pro. Kabudi
Kwa upande wake Balozi wa Vatican hapa Nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski amesema kuwa Vatican itaendelea kuimarisha mahusiano yake ya kidiplomasia na Tanzania kwa masuala yenye maslahi ya haki, utu, amani na utulivu.
“Maongezi yangu na Mhe. Waziri yalikuwa mazuri kwani tuliongelea masuala mbalimbali yenye maslahi kwa binadamu yakiwemo masuala ya kukuza diplomasia yetu pamoja na masuala ya amani na usalama duniani,” Amesema Askofu Mkuu Solczynski.
Katika tukio jingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Tate Olenasha amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria hapa nchini Mhe. Mhe. Ahmed Djellal ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu kuimarisha diplomasia baina ya Tanzania na Algeria.
No comments :
Post a Comment